JIBU..
Kuhadaa ni kudanganya yaani kutumia njia ya uongo/ ya mkato ili kiufanikisha jambo fulani…
Tunalipata neno hili Katika vifungu hivi,
Mwanzo 31:20 “Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia”
Mithali 12:5 “Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa”
Warumi 1:28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 1.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na HADAA; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya
2Petro 2:14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;
2Petro 2:18 Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
Tuangalie mifano halisi ya kuhadaa..
>Unaweza kuona mume wa mtu anaenda katika kumbi za starehe kucheza miziki ya kidunia na kulala na wanawake makahaba usiku kucha lakini nyumbani kwake amemuaga mke wake kuwa anasafiri, tayari hapa kamhadaa mkewe.
>Kuna wafanyabiashara ambao hutumia mizani kwa ajili ya kupimia bidhaa zao na wanapopima hupunguza uzito wa jiwe la mzani ili kupunguza kipimo lakini kwa bei ileile na mteja hupata upungufu fulani katika hiyo bidhaa au wengine huongeza bei zaidi ya bei elekezi iliyopo sokoni, hawa nao wanawahadaa wateja wao.
>Kutumia nafasi uliyonayo vibaya kwa manufaa yako binafsi, mfano ujuzi, elimu, karama, uongozi n.k.Yawezekana ukawa ni mchungaji, unawaambia watu Mungu kanipa maelekezo mtoe sadaka kwangu ili mpate kuponywa, tayari hapa umewahadaa watu wa Mungu kwa sababu neno linatuambia tumepewa bure basi na tutoe bure.
Kuwahadaa wengine sio jambo nzuri kwa sababu hii ni tabia ya ibilisi, huitumia kuwaangusha wanadamu katika dhambi kama alivyofanya katika bustani ya Edeni alipomhadaa Hawa kwa kumwambia wakila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya hawatakufa jambo ambalo sio sahihi.
Neno linasema shetani ni baba wa uongo, basi ikiwa na sisis tutaifuatisha tabia hii ya ulaghai tutakuwa tunaonyesha wazi kuwa tupo upande wa shetani. Kuhadaa ni matokeo ya wivu na kutopenda mafanikio ya wengine. Tukiwa na upendo ndani yetu tabia hii itaondoka hivyo yatupasa kulifuata pendo la Mungu.
Je dhambi hii inakuandama au dhambi nyingne yoyote? Basi Yesu ni msaada wako pekee, yeye hutuwezesha kushinda maisha ya dhambi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.