Tirshatha ni nini kama ilivyotumika kwenye biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Neno Tirshatha katika biblia tunalipata katika vufungu vifuatavyo..


Ezra 2:63 Na huyo Tirshatha akawaambia wasile katika vitu vitakatifu sana ,hata atakaposimama kuhani mwenye urimu na Thumimu.

Nehemia 8:9 Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa Bwana, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati

Nehemia 10: 1 Basi hawa ndio waliotia muhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;

Hili ni neno lenye asili ya kiajemi, maana yake ni mtawala aliyeteuliwa kuwa kiongozi katika uyahudi akiwa chini ya ufalme wa uajemi, mtu huyu hujulikana kama gavana au liwali, tunamuona Nehemia alikuwa Tirshata (Nehemia 5:18

Hata Zerebabeli aliwahi kuwa kiongozi katika nafasi hii Ezra 2:63, watu hawa walikuwa wakuu wa majimbo ambayo walipewa kuyaangalia na kusimamia kazi zote alizoagiza mfalme.


Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *