Fahamu mwandishi wa kitabu cha filemoni

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Kitabu Cha filemoni ni miongoni mwa nyaraka zilizoandikwa na Mtume Paulo huko kifungoni Rumi.

Waraka huu Paulo aliuandika kwa filemoni mtu aliyegeuzwa na injili yake mtume Paulo.

Baadaye filemoni anakuwa mtumishi wa Bwana katika nyumba yake mwenyewe, na kufanyika baraka kwa watakatifu katika kanisa la kolosai

Filemoni 1:2 “na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako”

Kilichomsukuma Sana mtume Paulo kuandika waraka huu ni kwa mtenda kazi mpya aliyemzaa katika Kristo jina lake Onesmo.

Hapo Mwanzo huyu Onesmo alikuwa mtumwa wake filemoni aliyemwibia vitu vyake na kukimbia. Sasa Paulo anamwambia filemoni ampokee na amchukulie kama Mtendakazi mwenzao katika Kristo, maana ametubu na yu tayari kwa Utumishi.

JE umempokea Yesu maishani mwako? Kama bado basi kuna maelezo hapo chini utayasoma kisha utawasiliana nasi

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *