FAHAMU MAMBO SITA AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUONDOA UOVU NDANI YA MTU.

Biblia kwa kina No Comments

 

 

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Baada ya kumwamini Yesu na kuokoka, kuna mambo sita Mungu huyafanya ili kuondoa ule uovu ndani ya mtu, Nayo ni..

1. DAMU
Kwakuwa sote tulizaliwa katika deni la dhambi, hukumu ya mauti ilikuwa juu ya Kila mmoja wetu (Rumi 6:23). Kwa kifo Cha Yesu Kristo msalabani deni hili lililipwa (Rumi 5:8) na sote tukapokea Msamaha wa dhambi Bure kwa Neema. Ni nani angalimpendeza Mungu kwa matendo yake? Hakuna! Bali sote tumeokolewa kwa Damu ya Yesu.

Baada ya kusamehewa dhambi, Na lengo la Mungu Atusamehe na tusiwe watumwa wa dhambi Tena. Tunawezaje kujiepusha na dhambi? Ni kwa hatua inayofuata..

2. NENO
Tukiwa kama Waamini au kanisa la Kristo, ni kwa neno la Mungu pekee ndipo tunajisafisha mavazi [matendo] yetu, kadri unavozidi kufanya Juhudi kutafuta maji haya ya Uzima[Neno] ndipo unavyozidi kujitakasa

Waefeso 5:26 ” ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.”

Neno Hilo limebeba maonyo, mafundisho, njia na Maagizo mbalimbali (2 Timoteo 2:16). Baada ya kuendelea kujifunza zaidi basi Pole pole mtu huanza kuziacha njia zake za awali za upotevu na kuanza kuona Hana hatia ndani yake kwa kufuata Yale Mafundisho ya neno la Mungu. Hutaweza kuwa safi pasipo Neno la Mungu, hivyo basi mpendwa, SOMA BIBLIA!

3. MOTO
Si Kila uchafu hutoka kwa maji mwingine huitaji moto kuuondoa, mfano uchafu unaoshika na kuganda pamoja na dhahabu haiwezi kutolewa kwa maji Bali kwa moto (kuuyeyusha).
Hata Mungu wetu pia hufanya hivyo kwa watoto wake , hutumia moto kuondoa uchafu Sugu ulioshindikana kuondoka kwa Neno, Sasa anatumia jambo au tukio Fulani la kimaisha kuliondoa Hilo; mfano iliyotumika kwa mfalme Nebukadreza kukaa miaka Saba porini kama mnyama ili kuondoa kiburi chake Sugu(Daniel 4)

1Petro 1:6 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”

4. FIMBO
Hii ni kawaida hata kwa wazazi wetu wa kimwili huturudia kwa fimbo ili kusisitiza juu ya Ujinga au makosa waliyotukataza, na kuonekana bado unarudiwa. Ni hivyo pia Hata kwa Mungu na watoto wake, soma

Waebrania 12:6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

7 ” Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?

8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?

10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.”

Soma pia
Mithali 22:15″ Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.”

5. PEPETO
turejee

Mathayo 3:11 ” Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

12 Ambaye PEPETO lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”

Pepeto hili la Yesu Kristo huondoa Yale makapi uliyotoka nayo Ulimwenguni. Hivyo kama inavyofanywa katika ngano kurushwa juu na chini kutikiswa ili tu kuruhusu makapi yaiache ngano ya kweli, na baada ya kuonekana ngano imejitenga basi mtu anakuwa shwari. Mfano Ibrahim anamtoa Uru, kukimbilia kanaani, misri, mara kurudishwa Lakini baadae tunaona Mungu anampa Pumziko baada ya wote waliokuwa nae kutoweka.

Sikiliza, kipindi Fulani katika wokovu wako unaweza pitia Hali ya kukosa utulivu, yaani kupata kukosa, kupanda au kushuka, angalia na usitetereke. Hiyo Hali haitokuwepo baada ya makapi kutoweshwa na upepo.

6. DAWA
Yesu ni Tabibu, wakati mwingine anajua yanayotokea yanatokana na magonjwa/ majeraha rohoni, hivyo anakutibu.

Baada ya hatua hii ndipo utaona yaliyokuwa yakimweka mbali mtu na Mungu wake yanakomeshwa mfano mapepo, madhaifu ya kimwili kama tamaa yanayofanya amkosee Mungu na mengine mengi katika maisha yake, na hatimaye atakuwa mwema. Na hatokuwa chini ya dhambi Ile Tena, yakiwa kama matokeo ya kutibiwa na huyu Tabibu mwema.

Tukisoma..

Ufunuo 3:18
“Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na DAWA ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”

Hivyo ikiwa umefanyika Mtoto wa Mungu tarajia hayo katika maisha yako. Haiwezekani ukawa Umeokoka angali hujabadilisha mienendo au matendo yako, Hilo SI kusudi la Mungu!

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *