Shalom.
Hakuna chakula kilichokatazwa, kwa maana kinachomnajisi mtu, si kinachoingia bali kinachotoka. Pia tuangalie nyaraka mbalimbali za mitume zimasemaje kuhusu hili..
1Timotheo 4:1-5 inasema..
“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”
Vyakula vyote ni halali vikiliwa kwa Moyo wa shukrani na IMANI, pia inaaswa anayekula asimhukumu asiyekula, maana tumetofautiana! Hatujaruhusiwa kuhukumiana kwa vyakula.
Lakini pia ni muhimu kuzingatia kutoudhiana kwa makusudi wakati wa kula vyakula hivyo ili kulinda Amani miongoni Mwa Kila mmoja.
Yaani tuwe wenye hekima tuwapo miongoni mwa Jamii au watu tofauti tofauti, tuangalie tusiwakwaze kwa Hilo, maana hakika tutakuwa tumemkwamza Kristo mwenyewe.
Tusome..
1wakorintho 8:13 inasema “Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.”…
8:8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu. “
Tuangalie na waraka kwa Warumi..
Warumi 14:14 “Najua, TENA NIMEHAKIKISHWA SANA KATIKA BWANA YESU, YA KUWA HAKUNA KILICHO NAJISI KWA ASILI YAKE, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.
15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. ”
Angalia, watu wamekuwa wakitumia Agano la kale kuhukumu vyakula, lakini kufanya hivyo sio sahihi! Maana kulikuwa na ujumbe au ufunuo fulani mbele ya Kila mnyama aliyekatazwa mfano asiecheua( asiyetafakari maneno ya Mungu), wasio na kwato, vilema n.k wote walikuwa ni fundisho kwa Wakristo wa Agano hili la rohoni, lakini alipokuja Kristo, Mungu alitakasa Wanyama wote (soma Matendo 10:10-15) na kutusisitiza sisi kutovitia unajisi.
2) kuhusu uvutaji sigara au kunywa pombe;
Ni kuuharibu mwili huu ambao si wetu. Mfano unapokunywa pombe, kutumia madawa ya kulevya, sigara, kuchora tattoo, uasherati, masturbation n.k vyote vinapelekea kuharibu miili yetu Ambayo ni hekalu la Roho Mtakatifu..
Soma..
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.