Fahamu maana ya “Roho za manabii huwatii manabii”

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Ili kupata taarifa sahihi, tufuatilie habari nzima kuanzia juu kidogo..

1Wakorintho 14:26 “Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.

28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.

29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.

30 Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.

31 Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.

32 NA ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII.

33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu”.

Kwa mtiririko huu inaonesha kuna hali ya machafuko ilizuka miongoni mwa watu wa kanisa la Korintho, yaani katika ibada Kila mmoja anataka kutoa UNABII, anataka kunena kwa Lugha, anawimbo wake, ufunuo wake n.k

Angalia, mfano kanisani kila mtu anazo karama zote na anataka zitumike na yeye, yaani afundishe, atoe UNABII, afasiri lugha, ahubiri nk.. vyote afanye mwenyewe, JE kutakuwa na hali katika kanisa? Ni dhahiri hakutakuwa na kujenga mwili wa Kristo tena Bali ni machafuko tu! Hivyo itakuwa ngumu kufanya kazi ya Mungu na kusikia sauti yake.

Sasa kutokana na hali hiyo kuzuka katika kanisa la Korintho, mtume Paulo anawaambia wasiwe na utaratibu huo, Bali ikiwa watu 20 au 10 wamepata mafunuo Fulani au unabii fulani, haipaswi wanene wote kwa Pamoja! Bali wapewe nafasi wawili au watatu na hao wengine wapambanue, ikitokea wale ambao hawakupata nafasi kung’ang’ania, basi wakumbuke kuwa “ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII”.

Akimaanisha ikiwa wao ni Manabii kweli, basi watii utaratibu uliokwisha kuwekwa na Manabii wenzao, maana Mungu si waachafuko Bali wa Utaratibu. Hata ikiwa yule aliyepata nafasi ya kutoa mafunuo, akiona mwenzie kapewa ufunuo mkubwa zaidi basi awe radhi kumpisha, ili wote kwa pamoja wafanye kwa kujenga kanisa na si kwa mashindano!

Utaratibu huu pia unapaswa ufuatwe nasi wakristo wa kanisa la sasa, ili tuujenge mwili wa Kristo na tutambue ya kuwa Mungu Wetu si wa machafuko bali wa Utaratibu.

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *