Shalom.
Isaya 42:19 “Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa Bwana?
20 Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii”.
Maneno ya Mungu kupitia nabii Isaya kwa Wayahudi, waliokuwa wa kwanza kumjua Mungu pamoja na Miujiza na Sheria zake na matendo yake makuu tangu Zamani za baba zao, ambao Sasa Mungu anawaita wajumbe au watumishi wake, lakini ndio wanakuwa vinara kugeukia miungu mingine, maovu kuliko hata wale mataifa wasiomjua Mungu.
Hivyobasi maneno haya hayamaanishi kuwa watumishi wa Mungu ndio vipofu na viziwi kama inavoonekana! Hapana Bali iliwalenga zaidi Wayahudi.
Hii ilionekana hata katika ujio wa [Masihi] Yesu Kristo, watumishi wa Mungu (mafarisayo, masadukayo, na waandishi) ndio walikuwa wa kwanza kumkataa, angali wao ndio iliwapasa wampokee maana walikuwa wakiujua UNABII na torati vyote kumhusu yeye, lakini wanakuwa vinara kumpinga na hatimae kutimiza UNABII kwa kumuua.
Tusome..
Yohana 9:39 “Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.
40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?
41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa”.
Unaweza kuliona hili katika injili za Leo, watumishi wa Mungu wanashindwa kutambua wokovu halisi aliouleta Yesu baada ya kufa na kufufuka (kuleta Uzima wa milele); lakini wanaitumia hiyo hiyo injili kujitafutia fedha na kujali kuhusu matumbo yao, bila kujali kazi ya Mungu ambayo ni wokovu kwa wanadamu.
Wanaacha wito wao wa kumtumikia Mungu na kugeukia Mishahara au Ulimwengu yaani Biashara, uchumi na ustawi wa fedha lakini wameacha mbali kabisa mambo ya kiroho yaletayo Uzima wa milele, na kugeukia ya Mwili Ambayo hatma yake ni mauti (Yohana 10:12-13)
Bwana Atusaidie tusiwe viziwi na vipofu! Tusirudie makosa waliyoyafanya mafarisayo na masadukayo. Hatimaye tubaki n kudumu katika Neno la Mungu.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.