Shalom, jina la Bwana libarikiwe.
Mithali 14:20 “Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi”
Angalia na hapa..
Mithali 19:4 Inasema “Utajiri huongeza rafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake”.
Hizi ni Mithali kama zilivyoandikwa na mfalme Sulemani kwa hekima alizopewa na Mungu, ameainisha mafunzo na maonyo mbalimbali kuhusu maisha ya kiroho na ya kimwili pia.
Lakini si kila Mithali ni Agizo! Zingine ulikuwa na uhalisia kuhusu Mambo Fulani aliyojifunza Sulemani katika maisha yake, mfano Maskini wanachukiwa, wanyonge hudhulumiwa; haya si Maagizo bali ni uhalisia wa mambo katika maisha yake Sulemani lakini si kwamba yalikuwa na Maagizo
Mfano pitia vifungu vifuatavyo..
Mithali 14:20 “Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi”
Pitia pia na hili..
Mithali 28:6 “Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri”
Sote tumeona, hakuna agizo lolote hapo! Bali ni uhalisia au kwa kiingereza “life experiences”. Katika maisha yake aliona matajiri hususani wadhalimu wakiwa na rafiki wengi (japo ni wasiofaa) na Maskini wakichukiwa vitu ambavyo ni dhahiri hata ukiangalia Leo yanatokea hivyo. Hivyobasi hayo SI Maagizo.
Anagundua jambo Hilo na sehemu nyingine mbalimbali..
Mhubiri 9:14 “Palikuwa na mji mdogo, na watu ndani yake walikuwa wachache; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.
15 Basi, kulionekana humo MTU MASKINI MWENYE HEKIMA, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo HAPAKUWA NA MTU YE YOTE ALIYEMKUMBUKA YULE MTU MASKINI.
16 NDIPO NILIPOSEMA, BORA HEKIMA KULIKO NGUVU; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.
17 Maneno ya wenye hekima yanenwayo taratibu husikiwa, Zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya wapumbavu.
18 Hekima NDIYO BORA KUPITA SILAHA ZA VITA; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi”
Tunaona akimsifia Maskini kwa kusema Hekima ni bora kuliko hata silaha za vita. Tuangalie pia na hapa..
Mithali 16:16 “Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha.
Anatuonesha jinsi Maskini alivyouokoa mji, pia anatuonesha kuwa IPO thawabu yake baada ya haya..
Mhubiri 4:13 “Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu”.
Sikiliza, Unaposoma Mithali na vitabu vingine vya hekima kama hivi vya Sulemani, uwe makini na uelewe vyema maana SI yote ni maagizo!
Tukirudi kwetu katika wito wa Ukristo, hatujaahidiwa marafiki na Mali nyingi, Bali tutachukiwa na wengi, lakini tusihofu maana huo ni muhuri wetu..
Luka 21:16 “Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.
17 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu”
Ametuahidi kuwa nasi katika vipindi vyote ambavyo tutavipitia tu, navyo ni dhiki za hapa na pale lakini hatotuacha..
Soma..
Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako NA UMASKINI WAKO, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.
10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”
Mathayo 16:2 “Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi”.
Ubarikiwe
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.