Biblia ilifunua nini kusema vipo sita Naam vipo saba?

Maswali ya Biblia No Comments

Swali: JE? Biblia Ina maana Gani kusema “vipo sita, naam vipo Saba” kwanini isingesema moja kwa moja tu kuwa vipo Saba?

Jibu: inayotumika hapo ni lugha ya Zamani inayotumika kuweka mkazo au msisitizo kuhusu lile jambo la mwisho, yaani Kama vinaonekana vinne, lakini kuna Cha tano ambacho ni muhimu zaidi.

Mfano tufuatilie maneno haya,

Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;

19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu”.

Angalia, yameandikwa mambo sita anayoyachukia Bwana, lakini anatumia lugha hiyo kuonesha kile cha Saba kuwa ni Cha msingi zaidi (kupanda mbegu ya fitina kati ya ndugu).

Soma pia..

Mithali 30:18 “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.

19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana”.

Utaona Tena anasema vinavyomshangaza ni vitatu, anatumia Tena lugha hii kuonesha mkazo kuhusu suala la nne (mwendo wa mtu pamoja na Msichana)

Rejea pia..

Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.

30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;

31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki”.

Pitia na mifano hii pia..

Mithali 30:15 “Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi!

16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!”

Soma

Ayubu 5:19 “Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.

Pitia pia amosi 1:4,

Amosi 1:3 “Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma”;

Pia yapo mambo saba yanayomkamilisha mwanadamu kibiblia, lakini lipo la nane ambalo ni muhimu zaidi nalo ni Upendo..

2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,

6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,

7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, UPENDO.

8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.”

Yote ni muhimu lakini tunapokosa Ule upendo wa Ki Mungu yaani wa Agape basi bado hatujakamilishwa.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *