DANIELI ALIKUWA WAPI WAKATI WENZAKE WANATUPWA KWENYE TANURU LA MOTO?

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu katika.

Tukisoma kwenye biblia hakuna mahali imeandika kwamba Daniel alikuwa wapi wakati wa tukio hilo linatokea la wenzake kutupwa kwenye tanuru la moto baada ya wao kukataa kuisujudia sanamu ya Mfalme Nebukadreza. 

Na hii ni kwa sababu biblia haichukui kila kitu na kukiandika bali inachukua matukio muhimu tu kwa ajili ya kutufundisha sisi hivyo tutakwenda kuangalia maeneo baadhi ambayo katika hayo huenda Danieli alikuwa katika moja ya hayo..

Au tunaweza tukasema sababu ambazo zilipelekea kutokuwepo yeye pale katika tukio lile.

 

  1. Sababu ya kwanza.

Huenda watu waliokuwa pamoja na mfalme agizo hilo halikuwahusu yaani waliokuwa katika jumba la Mfalme ukisoma vizuri utaona Mfalme Nebukadreza aliwaitwa wakuu wote aliokuwa amewaweka katika majimbo mbali mbali duniani Kote ili kupima/kuangalia utii wao mbele zake.

Kwa kuwaambia waisujudie ile sanamu yake.. Sasa kwa sababu Danieli alikuwa katika jumba la ufalme agizo hilo halikumhusu kabisa..

 

Danieli 2:49 “Tena, Danielii akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme”.

Hivyo kumbe wakina Sheldrake, Meshaki, na Abednego hawa woye walikuwa ni wakuu katika sehemu tofauti tofauti ulimwenguni Kote. Hivyo wao walitoka ila Danieli alibakia katika jumba la ufalme.

 

  1. Sababu ya pili.

Huenda wakati amri inatolewa Danieli mwenyewe hakuwepo tukisoma maandiko yanatuambia Danieli aliwekwa juu ya waganga wote duniani na wenye hekima,wanajimu nk

Danieli 5:11

“Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;

 

3.Sababu ya mwisho.

Tukisoma toka mwanzo kabisa Danieli alikuwa na misimamo yake ambayo kwa hiyo haikuweza kubadilishwa na mtu mpaka anakufa..

Alisimama thabiti katika imani yake pasipo kuteteleka hata kidogo. Hata wakati wanapewa Divai na vyakula ambavyo vitawatia unajisi yeye Danieli alivikataa lakini pamoja na wenzake hivyo hivyo walikataa kujitia unajisi kwa vyakula hivyo.. (Danieli 1:8-16 inaeleza vizuri soma..)

Huenda kukawa pia na uwezekano kabisa Danieli alimwambia Nebukadreza msimamo wake. Na akamuelewa ndio maana hakuhusishwa juu ya jambo hilo.

Lakini sio kwamba Danieli alikubali kufanya vile ndio maana akawa sawa la! Maana alikuwa radhi kutupwa kwenye tundu la simba kwa sababu ya kutokuacha kumuomba Mungu wake japokuwa amri ilitoka lakini alikuwa tayari kwa lolote..

TUNAJIFUNZA NINI KATIKA HABARI HII?

Kuna nyakati Mungu atatuepusha na mambo mabaya au majaribu  ambapo nafasi ya kuyakwepa ni ndogo mno. Lakini upo wakati ambao Mungu ataruhusu upite katika majaribu mazito ili kuangalia Je bado utaendelea kushikamana nae? Kama vile Mungu alivyoruhusu Danieli atupwe kwenye tundu la Simba..

Hivyo hivyo na sisi hatuna budi kuwa na msimamo katika nyakati na majira yote juu ya Mungu wetu wala tusitikisike kwa lolote..

Ubarikiwe sana. 

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *