Fahamu maana ya hili andiko, 1petro 3:20-21

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom..

Je unajua kuwa ubatizo unaweza kuua lakini pia unaweza kuokoa?

Kuna jambo kubwa limejificha katika ubatizo lakini kama watu wangelijua jambo hilo bila shaka wangefanya bidii kuutafuta ubatizo.

tusome vifungu vifuatavyo

1 Petro 3:20 “watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, WALIOKOKA KWA MAJI.

21 MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO, UNAOWAOKOA NINYI PIA SIKU HIZI; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo”.

Katika vifungu hivyo kuna mambo matatu tutayaangalia…, tutaangalia jambo moja baada ya lingine.

1.WATU WANANE WALIOKOKA KWA MAJI

Jambo la kwanza tunaloliona hapa ni kwamba ‘maji ni njia ya wokovu’. Watu wanane yaani Nuhu, mkewe, watoto wake watatu na wake zao waliokoka kwa maji. Wale ambao hawakuamini injili wakati huo waliangamizwa kwa maji na maji hayo hayo yalimwokoa Nuhu na ghadhabu ya Mungu.

2.MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO, UNAOWAOKOA NINYI PIA SIKU HIZI

Wakati ule Nuhu aliokoka kwa maji na wakati huu sisi pia tunaokoka kwa maji, yaani kwa njia ya kubatizwa. Na Bwana Yesu alisema katika Marko 16:16 ‘Aaminiye na kubatizwa ataokoka‘ kumbe kuamini peke yake haitoshi, ubatizo ni muhimu.
Habari za gharika wakati wa Nuhu zinatupa ufunuo wa ubatizo.

Yawezekana hata Yohana mbatizaji alipata ufunuo wa ubatizo kutokea hapo. Kumwamini Yesu ni sawa na kuingia ndani ya safina, unapobatizwa ubatizo wa kuzamishwa katika maji mengi kisha ukaibuka juu ni sawa na kuingia ndani ya safina wakati wa gharika na kutoka salama.

Baada ya gharika Nuhu aliingia katika ulimwengu mpya na kuanza maisha mapya na kuyaacha yale maisha ya shida, dhuluma na maasi ya kila namna yaani uchafu wote wa kwanza haukuwepo tena.
Sisi pia tunapobatizwa katika ulimwengu wa roho tunaondolewa uchafu wote tuliokuwa nao,yale maisha ya dhambi yanapotea kabsa. Hii ni faida kwetu ambayo pia inatupeleka katika jambo lingine la tatu na la mwisho.

3.SIYO KUWEKA MBALI UCHAFU WA MWILI, BALI JIBU LA DHAMIRI SAFI MBELE ZA MUNGU.

Mtu anapobatizwa si kwa ajili ya kuondoa uchafu wa mwilini kama vile jasho au vumbi, lengo kuu ni kuondoa uchafu wa rohoni na ubatizo huo ndio jibu la dhamiri zetu safi mbele za Mungu.

Je tayari umebatizwa ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la Bwana Yesu kama isemavyo Matendo 2:28?

Ikiwa bado hujafanya hivyo usiendelee kusubiri, sasa umejua faida zake basi baada ya kumwamini Kristo basi kwa namna yoyote tafuta ubatizo huo sahihi upate kuokoka.

Bwana akubariki.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *