FAHAMU KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO.

Biblia kwa kina No Comments

Bwana Yesu asifiwe ndugu katika Kristo Yesu.  Karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu. 

Pale tunapookoka na kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu. 

Sasa Roho Mtakatifu ndani yetu anafanya kazi nyingi zaidi ndani yetu na tunaposoma maandiko yanasema ni MSAIDIZI. Maaana yake anatusaidia pale tusipoweza anasimama nafasi hiyo katika kutukamilisha. Kabla ya kwenda katika kiini cha somo Letu tutajifunza msaidizi ni mtu wa namna gani..

Msaidizi ni mtu anaefanya kazi ya mwingine. Au kazi za mtu mwingine.

Maana yake maana yake anafanya kazi za mtu ambazo alitakiwa azifanye yeye lakikutokana na udhaifu hawezi kuzikamilisha zote hivyo Msaidizi anamsaidia mahali asipoweza.

Sasa hii ni maana ya kawaida kabisa lakini katika upande wa Roho Mtakatifu katika utendaji kazi ndani yetu ni zaidi ya hapo. Tutakwenda kujifunza kwa ufupi tu kazi za Roho Mtakatifu ndani yetu. Na ni vyema kama watu tuliozaliwa mara ya pili kuyatambua mambo haya yatatusaidia sana.

Sasa ukisoma katika SUV(Swahili union version) imemtaja Roho Mtakatifu kama Msaidizi peke yake. Tusome..

Yohana 15:26“Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.”

Unaona hapo? Inamtaja kama Msaidizi. Ambae huyo atamshuhudia Yesu Kristo.

Lakini tukisoma katika biblia ya kiingereza..

Amplified Bible imeelezea kwa undani zaidi.  Tusome..

John 15:26

[26]But when the Comforter (Counselor, Helper, Advocate, Intercessor, Strengthener, Standby) comes, Whom I will send to you from the Father, the Spirit of Truth Who comes (proceeds) from the Father, He [Himself] will testify regarding Me.

Inamuita Comforter maana yake MFARIJI. Lakini imeendelea kusema maneno sita ndani yake na yote yenye maana tofauti tofauti  ambayo leo tutatwenda kuyatazama moja baada ya jingine ambayo ni

Counselor,Helper, Advocate,Intercessor,strengthener na Standby. 

MAANA HALISI YA MANENO HAYO. 

Ni maombi yangu kwa Bwana wangu Yesu Kristo uelewe zaidi ya hiki kilichoandikwa..

1.Counselor. Maana yake ni mshauri.

Kazi moja wapo kubwa ya Roho Mtakatifu ndani yetu ni kutushauri. Tunapokuwa katika vipindi vigumu na katika hali ya kukata tamaa na kuona hakuna namna tena Roho Mtakatifu ndani yetu anafanya kazi hiyo kwa upole kabisa.  Roho Mtakatifu alikuwa juu ya Bwana wetu Yesu Kristo na ndio aliekuwa anafanya kazi ndani yake 

Isaya 11:2“Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya SHAURI na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;

2 Helper. Maana yake ni Msaidizi.

Anatusaidia mahali tunapokuwa ni wadhaifu hatuwezi kutembea au kuenenda sawa sawa na mapenzi ya Mungu basi yeye anasimama katika nafasi hiyo Anatusaidia haleluya…. Katika mambo tusiyoweza kuyashinda basi yeye anasimama na anatupa nguvu ya kuyashinda..

Pia anatusaidia kuomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu (kuomba katika Roho) ambapo pasipo Roho Mtakatifu hakuna anaeweza kuomba sawa na mapenzi ya Mungu/katika Roho.. maana maandiko yameweka wazi hilo kuwa “hatuwezi kuomba jinsi itupasavyo.”

Warumi 8:26“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”

3. Advocate Maana yake ni Mtetezi.

Anasimama kututetea vivyo hivyo mbele za Mungu Shetani anapopeleka pia mashtaka yake Roho Mtakatifu anatutetea na tunaonekana hatuna hatia mbele za Mungu. Ni muhimu sana kulifahamu jambo hili.kama vile wakili anaposimama mbele ya mahakama kutoa utetezi juu ya mtu alietiwa hatiani kwa kosa fulani vivyo hivyo Roho Mtakatifu anafanya ( yaani Mungu mwenyewe ndio anaekutetea Haleluya….atukuzwe Bwana Yesu). 

4 Intercessor.  Maana yake ni Mwombezi.

Roho Mtakatifu mwenyewe anatuombea usiku na mchana mbele za Mungu (ni upendo wa namna gani huu?, Mimi na wewe tunamlipa nini??)Hakika Yesu  ni mwema sana..( Warumi 8:34) mahali tunapokuwa kwenye shughuli zetu, tumelala yeye halali akituombea na tunaepushwa na mambo ya kutisha mno kwa maombi yake(pia inakupasa uwe muombaji sana..)

5. Strengthener. Maana yake Mtia nguvu/Muimalishaji.

Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kutuimarisha ndani yetu. Mahali ambapo hatuna nguvu anatutia nguvu tutazidi kuwa imara na anazidi kitukamilisha zaidi.(Wafilipi 4:13)

 

6.  Standby. maana yake anaesubiri na alie tayari kufanya jambo lolote/kutoa msaada.

Roho Mtakatifu anatamani kutusaidia zaidi ya sisi tunavyotamani atusaidie. Yuko tayari wakati wowote/muda wowote kutusaidia kitu chochote tunachohitaji. (Litambue hili..) yupo tayari lakini sisi ndio hatuko tayari. Na utayari wetu sisi ni kuomba na kusoma neno tunapofanya mambo haya kila siku basi Roho Mtaalamu anakuwa tayari kutupa msaada wowote ule tunahitaji…

Kumbuka haya yote yanahitaji utii wako na kumpa nafasi zaidi ndani yako hatakulazimisha kukushauri,kukusaidia,nk ikiwa hujibidiishi katika kuomba, kusoma neno,kushuhudia.nk 

Yaweke akilini mwako na katika roho yako na share na wengine pia baraka zi pamoja na wewe.

Maranatha. 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *