Fahamu maana ya  Mithali 10:25 (JINSI YA KUSHINDA VISULISULI KATIKA IMANI).

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Mithali 10:25“Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena; Bali mwenye haki ni msingi wa milele.

Kisulisuli kwa jina lingine tunaweza kusema ni kimbunga. Ni upepo ambao huwa unajikusanya sehemu moja na kutengeneza kitu mfano wa nguzo kwenda juu.

Sasa ili tuweze kupata maana vizuri katika mstari huu ni kipi alichokuwa anakimaanisha mwandishi wa Mithali hii.

Turejee mfano ule ambao Bwana Yesu aliutoa katika kile kitabu cha Mathayo..

Ambapo alikuwa anazungumzia watu wanaosikia maneno yake(injili halafu hawayatendi/ kuyafanya.).

Mathayo 7:24  Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

26  Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Sasa ukisoma kwa makini katika Mithali 10:25 utaona vyema kuwa mtu anaezunguziwa hapo asiye haki ni nani.

Ni mtu anaesikia injili ya Kristo na Haitii anaendelea na mambo yake tu. Ni Mkristo anaeenda kanisani na anasema “nimeokoka” lakini hakuna badiliko lolote katika maisha yake ya wokovu bado ni yule yule hataki kubadilika ndani yake. Sasa mtu wa namna hii hana tofauti na mpagani ambae hamjui Mungu kabisa. Wote hao wanaitwa ni watu wanaohitaji neema ya Kristo wako dhambini bado.

Sasa mtu wa namna hii anaonekana kwa nje ni Mtakatifu anaemtumikia Mungu lakini sivyo ndani yake bado anaendelea na uzinzi,uangaliaji wa picha za uchi,mlevi wa sirisiri.nk Sasa watu wa namna hii huwa wanaonekana kama wamesimama..

Lakini wanapopita katika majaribu madogo tu wanarudi nyuma kabisa ndio hicho Kisulisuli kikipita kama vile shida,udhia,wanarudi nyuma wanakuwa kama watu ambao hawajawahi kumjua mwokozi kabisa ni kwa sababu mioyo yao haikuwa kwa Yesu Kristo kabisa. Wengine wanapopata tu kitu fulani kama vile Fedha,biashara,Masomo nk wanamuacha Kristo.

Lakini mtu yule anayesikia maneno ya Kristo na kuyatenda mtu wa namna hii huitwa msingi imara uliojengwa juu ya mwamba (msingi wa milele) mtu wa namna hii tumaini lake linakuwa kwa Mungu siku zote na hata visulisuli vile kwa namna gani hawezi kutikisika kama maandiko yanavyosema..

Zaburi 125:1Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.”

Je unayashika maneno ya Yesu unapoyasikia? Kumbuka ili uweze kusimama, misingi yako iwe juu ya mwamba huna budi kufanya bidii katika kuyasikia maneno ya Kristo na kuyatenda. Uwe ni mmoja wa msingi ule wa milele. 

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *