Shetani ana uwezo wa kushusha moto kutoka Mbinguni?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom! jina la Bwana wetu yesu kristo lipewe sifa karibu mwana wa Mungu tujifunze maneno ya uzima.

Tunaweza kusoma kitabu hiki hapa chini.

Ayubu 1:14 “Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari”.

Hapo mwanzo Ayubu na watumwa wake hawakujua kuwa shetani ndiye anayewajaribu Bali alijua kuwa ni Mungu ndiye aliyekuwa anawajaribu japo hakujua sababu ya majaribu Yale kumpata pia kwa marafiki zake walijua kuwa Mungu kaushusha moto kuteketeza wale Kondoo na kumpiga ayubu mapigo na ndiyo maana yule mtumwa aliutaja moto kama umetoka kwa Mungu.

Mungu alipomtokea ayubu katika upepo wa kisulisuli na kumfunulia jambo lililoendelea rohoni jinsi ambavyo shetani alivyopeleka mashitaka kwa Bwana dhidi ya ayubu ndipo ayubu alipojua kuwa hayo yote yamesababishwa na shetani. tunaona Ayubu alisema hivi

Ayubu 1:21 “akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA; jina la Bwana na libarikiwe”.

Hapo aliposema Bwana ametoa na Bwana ametwaa tunajifunza nini?

Tunaweza kupitia majaribu tukadhani ni Mungu kumbe ni shetani isipokuwa hayo majaribu yanatupata baada ya Mungu kutoa kibali kwa shetani kuwa tujaribiwe au la! Na majaribu yamegawanyika katika sehemu mbili nazo ni hizi.

1.Majaribu ya shetani kwa mtakatifu

Ikiwa unayo Imani kama ya ayubu na ukapitia matatizo kama magonjwa, taabu, dhiki n.k basi fahamu kuwa Mungu kamruhusu shetani hivyo usiogope kwakuwa mwisho wako utakuwa ni mzuri kama wa Ayubu.

2.Majaribu ya shetani kwa mtu ambaye hajaokoka.

Kama haujampokea yesu utajikuta upo katika majaribu mazito kama misiba, magonjwa, mateso,n.k jua Mungu kamruhusu shetani akuletee hayo matatizo ili ugeuze moyo wako umrudie Bwana lakini usipotii kwa kutubu na kumrudia Bwana utakufa kwakuwa shetani anataka ufe katika dhambi na mateso.

Hivyo mpokee yesu ili akusafishe na upokee kipawa Cha roho mtakatifu ili ulinzi wa kiMungu uongezeke juu yako.

Hivyo shetani ndiye aliyeuleta ule moto na siyo Mungu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *