NIFANYE NINI NINAPOKATA TAMAA?

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Kama wanadamu tunaoishi rohoni na mwilini pia ni wazi kuna mambo mengi sana yanatokea ya kutukatisha tamaa na kuona kana kwamba wakati mwingine Mungu yupo mbali na si au ametuacha lakini je ni kweli?, jibu ni la si hivyo Mungu siku zote yuko pamoja na sisi na hatutakiwi kuogopa wala kukata tamaa.

Ndio maana sehemu nyingi sana Mungu anatwambia USIOGOPE. Kwa sababu hofu siku zote inaleta kukata tamaa na kuona kuwa haiwezekani.

 

Lakini Mungu anataka sisi tuwe kama jinsi watoto walivyo. Watoto siku zote hawakati tamaa wala hawachoki kama vile mtoto anavyo jifunza kutembea anaanguka lakini hakati tamaa anainuka tena na hakuna hata siku moja anakata tamaa.

mpaka anafanikiwa kutembea na anakuwa anaweza hata kukimbia na hiyo imetokana na jitihada za yeye kutokukata tamaa katika kuanguka kwake kule hakupoteza matumaini aliamini anweza kutembea.

Kama angelikata tamaa basi asingeliweza kuinuka nakutembea kabisa.

Pia na sisi Mungu anataka tuwe ni watu wa hivyo tunaponguka katika jambo Fulani tusikate tamaa na kuona hatuwezi kabisa la! Bali tuendelee hivyo hivyo mwisho wa siku utaweza kusimama na kukimbia.

Unatamani kuishi maisha matakatifu usikate tamaa pale unapoanguka katika dhambi, amka uendelee mbele huku ukijifunza kutokana na makosa kwa kugeuka kweli kweli na kuendelea mbele wala usiangalie na kutafakari jinsi ulivyoanguka na ukaona ya kuwa Mungu amekuacha..

Mungu yuko pamoja na wewe na lengo lake uamke uendelee mbele zaidi si ukate tamaa na  kubaki pale pale.

Sasa ili ushinde na uweze kuwa na amani pale hali ya kukata tama inapokuja kutokana na masumbu ya namna mbali mbali kama vile magonjwa,uchumi,kutengwa na ndugu/marafiki, kuona umefanya jambo Mungu amekuchukia na hawezi kukusamehe nk fanya mambo haya makuu manne(4) na hakika utaona unaendelea mbele zaidi. yafanye kuwa ni sehemu ya maisha yako.

MAMBO YA KUFANYA UNAPOKATA TAMAA.

 

  1. TAFAKARI UKUU NA UWEZA WA MUNGU.

Wakristo wengi wanakata tamaa kwa sababu wanakuwa ni wavivu wa kutafakari uweza na ukuu wa Mungu. Siri hii Daudi aliitambua vyema na katika nyakati zote ngumu alizokuwa anapitia basi alikuwa akitafakari uweza na ukuu wa Mungu matendo yake makuu aliyoyafanya na anajikuta anajenga imani ndani yake na kusimama na kuendelea mbele hata kupigana vita na kushinda.

Zaburi 77:11-15 “Nitayakumbuka matendo ya Bwana; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. 

12 Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. 

13 Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu? 

14 Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa. 

15 Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu. 

Tafakari kazi za Bwana alizozifanya jinsi alivyokuumba, akaumba wanyama na kila kitu na kukipa ufahamu na akili nk tafakari wokovu aliotupatia wanadamu nk .hivyo unapokakaa katika kutafakaro iko nguvu kubwa sana ya kusonga mbele katika kutafakari.

Usiwe ni mvivu wa kutafakari kabisa maana katika kutafakari iko njia na majibu utampa Roho Mtakatifu nafasi ya kusema na wewe.

 

2. SOMA NENO LA MUNGU.

Katika mambo ambayo hutakiwi kuyakwepa kama mwamini ni kusoma neno la Mungu, maana ndio chakula cha roho yako na ndio litialo uzima katika roho yako. neno linakupa matumaini na kukutia nguvu pale unapokuwa umechoka na kukata tamaa. Kumbuka neno la Mungu siku zote li hai. Linatusafisha na kututakasa kabisa.

Waebrania 4:12” Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”

Unaposoma neno utakutana na watu ambao nao walikosa kama wewe na wakamrudia Mungu na akawarehemu maandiko yanasema yeyeni mwingi wa rehema nk hivyo neno litakutia nguvu sana na utajifunza mambo mengi na utaimalika sana sana. USIIPUZIE WALA KUWA MZEMBE KUSOMA NENO.

Litakukumbusha wewe ni nani na unatakiwa ufanye nini na uishije.

3.OMBA/KUWA MUOMBAJI.

Hii ni sehemu ya maisha yako kama mwamini. Ni pumzi inayokupa nguvu ya kwemda mbele maana Neno bila maombi ni sawa na gari zuri lisilokuwa na mafuta haliwezi kutimiliza mahitaji ya watu kama kuwasafirisha kuwapeleka mahali Fulani.hivyo tambua kama mwamini maombi ni muhimu sana.

Ndio sehemu pekee unayokwenda kuongea na Mungu ana kwa ana na Mungu kusikia haja zako. Ndio sehemu unayofarijiwa na kuendelea mbele zaidi mahali ambapo ulikuwa huwezi. Maombi yanakufanya kuwa mtu wa tofauti kabisa na yanakuimalisha sana. Maombi yanakufanya pia uepushwe na majaribu.

Leo hii unalia unataka kumjua Mungu na hutaki kuomba na kusoma neno hutaweza..unataka Mungu akutie nguvu na huombi ndugu haiwezekani utakata tamaa na utarudia kuwa mtu wa kawaida kabisa na Mkristo asiekuwa na matunda. Anza kujizoesha kuomba. “MAOMBI SIO KARAMA” ni kwa kila mtu aliemwamini Yesu anawajibu wa kuomba.

4.MSIFU MUNGU.

Kuwa ni mtu wa kumwimbia Mungu katika nyakati zote katika sifa iko nguvu ya ajabu mno.penda kusikilza nyimbo za kumsifu Mungu na kumtukuza yeye.. na imba kwa kinywa chako unaposikiliza pia imba usikae kimya kwamba unaimbia moyoni ndugu. Hutaona nguvu yoyote fuatisha yale maneno utaona Bwana anakugusa kwa namna ya ajabu mno.

Umewahi kutafakari kwa nini Daudi alikuwa anapenda sana kumwimbia Mungu na kucheza? Kwa sababu sifa zile zilikuwa zinauinua Moyo wa Daudi katika kumtumainia Bwana.

 

Zaburi 59:16-17 “Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu. 

17 Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu”

Hivyo kuwa ni mtu wa kumwimbia Bwana kwa kinywa chako utaona jinsi Mungu anavyokuwezesha na kukuinua tena. Usiwe msikiliaji wa nyimboza kidunia hazikujengi zinakubomoa. Sikiliza nyimbo zinazomtukuza Mungu.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *