Je! Utoaji wako unamgusa Mungu?
Sehemu ya 01.
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima..
“Kuna utoaji unaomgusa Mungu na usiomgusa Mungu “ katika maisha ya Kikristo utoaji hasa kwa Mungu wetu ni wajibu wa kila mmoja mmoja wetu. Na anaetakiwa kufanya hivi si tajiri peke yake la! Bali kila mmoja wetu anakitu cha kutoa kwa Mungu.
Hivyo unaweza ukatoa katika utoaji wako lakini using usimguse Mungu kabisa hata kama umetoa mamilioni ya fedha.
Sasa ni utoaji upi hasa unaomgusa Mungu? Kupitia somo hili tutajifunza na kama ukifuata na kutendea kazi utaanza kuona mabadiliko ya maisha yako kupitia utoaji wako..
Somo hili ni muhimu sana kwa Mkristo yeyote ulimwenguni hivyo ni vyema ukajifunza kanuni ambazo unatakiwa kuzifuata..
Siku zote utoaji unaomgusa Mungu ni utoaji anaoutakabari/kuukubali Mungu na unamanufaa pia kwa mtu huyo anaetoa ni dhahiri mtoaji huyo lazima atabarikiwa tu. Kama utoaji unaotoa hauna manufaa basi bado kuna mahali utoaji wako haujamgusa Mungu na ndio maana ni muhimu sana ujifunze itakusaidia.
Na utoaji unaomgusa Mungu si kiasi cha fedha kingi sana unachotoa la! Utoaji haupimwi kwa namna hiyo kwa Mungu wetu.. Bali ni moyo wa mtoaji na namna anavyotoa kutoka ndani ya moyo wake.
Na zaidi sana Mungu ndio mwanzilishi wa utoaji katika ulimwengu huu. Dunia na vyote vikjazavyo ni mali yake/ni matokeo ya utoaji wake. Maandiko yanasema vyote vilitoka kwake (Yohana 1:3) utaliona hilo pia Soma (Mwanzo 1:31).
Pia katika maandiko wapo watu wengi ambao utoaji wao ulimgusa Mungu na utoaji wao ulikuwa na faida/Matokeo kwao kama vile utoaji wa Habili (Mwanzo 4:4) utoaji wa Ibrahimu (Mwanzo 22).
Wapo watu wengi tutazidi kuwatazama na ukisoma vizuri utaona mwitikio wa Mungu kwa hao watu baada ya kutoa baraka nyingi ziliambatana nao kwa sababu utoaji wao ulimgusa Mungu.
Utoaji siku zote umefungwa katika kanuni ulimwengu huu unaongozwa na kanuni vivyo hivyo mambo ya rohoni yanaongozwa na kanuni..
Na tutaziangalia kanuni hizi kwa undani hasa leo tutatazama kanuni moja Mungu akitupa neema tutatazama kanuni ya pili mpaka ya mwisho.
Lengo kubwa la somo hili ni kuchochea huduma ya utoaji ndani yako itayokuwa na matokeo kwako lakini pia itakayokuwa na matokeo katika mwili wa Kristo.. kanuni hizi zikawe msaada kwako na Mungu akusaidie.
Utoaji umefungwa katika kanuni hizi..
1.kanuni ya Umiliki.
Kanuni namba moja inayougusa moyo wa Mungu ni kanuni hii ya umiliki. Ukweli ni kwamba kila kiumbe hai kiliumbwa ili kitoe.
Kanuni ya asili ya uumbaji Mungu aliumba kila kitu kitoe kwaajiri ya manufaa ya kitu kingine. Vitu vingi tunavyoviona leo hii vipo vingine ambavyo hakuviumba kabisa.
Katika uumbaji wake Mungu hakuumba magari,ndege,fedha,kompyuta,Fridge,simu nk lakini Vitu hivi vilitaka wapi? Kama Mungu hakuviumba? Ukweli ni kwamba Mungu aliweka rasilimali zinazotumika kutengeneza vitu hivi ndani ya vitu vichache alivyoviumba..
Mwanzo 1:11-12 “Mungu akasema, nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.”
Ukisoma hapo utaona Mungu anaamuru ardhi itoe majani Miche na miti ya matunda nk maana yake aridhi ilipewa umiliki wa vitu hivi.
“utoaji ni tabia ya asili ya uimbaji wa Mungu kila kitu kiliumbwa ili kitoe”
Sasa utoaji ni nini?
Utoaji ni tendo la hiari la kuhamisha haki ya umiliki wa vile alivyonavyo mtu kwenda kwa Mungu au mtu mwingine.Mwanadamu aliumbwa na asili ya utoaji ndani yake.
Hivyo asili ya mwanadamu ni mtoaji tangu kuumbwa kwake kwa namna gani?
Mwanzo 3:6 “Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.”
Unaona hapo anasema “…..Akampa na mumewe naye akala.” Swali la kujiuliza ni nani alimfundisha Hawa kwamba ilimpasa kumpa pia Adamu ale? Hapa tunaona Hawa anahamisha umiliki wa lile tunda kwa mumewe..
Ukisoma mwanzo 4:4 Habili na kaini ni nani aliewafundisha kutoa? Soma pia Mwanzo 14:20 ni nani aliemfundisha Ibrahimu kutoa fungu la 10? Ni wazi kabisa utoaji ni asili ya mwanadamu.
Hatuoni mahali popote katika uumbaji Mungu anatoa sheria lazima watu wamtole sadaka la! Bali wenyewe walikuwa wanajua nini wafanye.. Sasa ukiangalia ni tofauti na siku za leo utoaji umekuwa ni kitu kigumu kwa nini?
Tuna kila kitu cha kutoa wala hakuna mtu ambae hana kitu cha kutoa.. tunaweza kumtolea Mungu vitu vingi vikiwemo.
1.Roho Zetu.
Mungu kila mmoja kamba kitu kikubwa sana ambacho ni roho zetu wenyewe na ndio kiunganishi kikubwa kati yetu sisi na Mungu tukitaka kushikama kwa uthabiti na Mungu ni lazima tuzotoe roho zetu kama sadaka kwake(kumbukumbu la Torati 6:5)
2.Mioyo yetu.
Ukisoma kwenye kumbukumbu la Torati 6 hapo amesema moyo na maandiko yanatwambia ndiko zitokako chemichemi za uzima (Mithali 4:23)Katika moyo ndipo palipo na utashi (akili), maamuzi na hisia. Kitu chochote tunachoweza kutoa lazima kianzie moyoni.
3.miili yetu.
Hazina nyingine tuliyopewa na Mungu ni miili yetu ambayo ina nguvu nyingi na tunatakiwa kuitoa miili yetu Km sadaka mbele za Mungu kwa ajili ya ufalme wake na tukifanya hivyo kwa uaminifu tutamuona Mungu katika viwango vingine maandiko yanasem.. (Warumi 12:1-2).
4.Muda.
Kila mwanadamu anamiliki masaa 24 kwa siku na rasilimali muhimu sana tuliyonayo ni muda.. ndio maana maandiko yanatutaka kuukomboa wakati. Tunatakiwa kuutoa muda wetu kwa ajiri ya ibada,kuwashudia wemgine,kuomba nk.
5.Mali zetu,Fedha nk
Maandiko yanasema muhesimu Mungu kwa mali zako hivyo haihitaji tuwe na mbilioni ya fedha la bali katika kidogo tulichonacho tumtolee Bwana siku zote..
“Mungu ni Mungu wa kanuni, siku zote hawezi kukutaka utoe kama hajakupa cha kutoa.”
6.ujuzi wetu.
Ikiwa haujaelewa zaidi katika kanuni hii ya kwanza basi katika kanuni ya pili na kuendelea naimani kuna kitu kikubwa Zaidi utajifunza katika sehemu ya pili…
Bwana Yesu akubariki sana.
Nimekuombea na ni Imani yangu Bwana azidi kukufungua macho juu ya jambo hili.
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.