Kutahayari ni nini kibiblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze maneno ya uzima kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Maana ya kutahayari ni kuaibika yaani kufanya au kufanyiwa jambo au tendo ambalo mwishowe huwa ni aibu jambo hilo ni kama kutukanwa, n.k.

Neno la Bwana linasema hivi

2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli”.

Katika hili neno Mungu anasema usiwe na aibu katika kuitangaza na kuisema kweli ya Bwana kwa mfano unakuta mtu ni mzinzi, mwizi, mlevi na matendo mengine mabaya mfano wa haya, alafu  anakosa ujasiri wa kumhubiria mtu mwingine kuhusu dhambi kwakuwa unakuta mtu huyo mwenyewe ni mtenda dhambi neno la Mungu linasema.

2Wakorintho 7:14 “Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli”.

2Wathesalonike 3:14 “Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari”;

Ayubu 11:3 “Je! Majivuno yako yawanyamazishe watu wawe kimya? Nawe hapo ufanyapo dhihaka, je! Hapana mtu atakayekutahayarisha”?

Isaya 50:7 “Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya

Hivyo tunapokuwa katika wokovu na kuwahubiria watu inatupasa tusiwe na mawaa yatakayo tufanya tushindwe kiwahubiria watu bali tuwe kielelezo kwa wasiookoka ili warejee kwa kristo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *