Amini anakukamilish.
Bwana Yesu hakuja ulimwenguni kufa kwa ajiri ya kutondolea dhambi tu kisha kutuacha. Kusudi kuu la Yesu Kristo kweli ni kutuondolea dhambi(kutuweka huru) lakini haiishii hapo tu bali yeye anatukamilisha na kazi ya kutukamilisha ni ya kwake yeye wala sio sisi..
Hatujikamilishi sisi wenyewe bali yeye ndio anatuwezesha. Labda utajiuliza kukamilishwa kwa namna gani au maana ya kukamilishwa ni nini maana yake?.
Kitu anachokitarajia Yesu Kristo mwisho wa siku kukiona kwetu ni sisi kufanana na yeye. Kama maandiko yanavyosema..
Warumi 8:29“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.”
Mtume Paulo hapa anafundisha watakatifu aaliokuwa Rumi kuwa kusudi la Mungu sisi tufanane na Kristo yaani tabia zetu,mawazo Yetu, maisha yetu mtu anapotutazama anamuoma Kristo ndani yetu ndio maana halisi ya “sio mimi tena Kristo ndani yangu” Yesu anataka tufukie katika hatua hii.
Na hii yote sio kwa nguvu zetu ni yeye anayefanya sisi kazi yatu ni kutii na kuenda sawa sawa na anavyotutaka tuenende.
Ukisoma pia..
2 Wakorintho 3:18 “Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.”
Mtume Paulo hapa anawafundisha watakatifu walio kuwa Korintho katika waraka wake wa pili.. kwamba.
Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yetu kutubadilisha tufanane na Kristo hatua kwa hatua.. Haleluya.
Usiogope na kuanza “kufikiri sana itawezekanaje?, mbona sioni mabadiliko yoyote?, niko vile vile tu, nahisi hii ni ngumu sana sidhani kama itawezekana nk”
Ndugu yangu ondoa kabisa mawazo haya na ufahamu huu ndani yako amini Kila siku Yesu Kristo anafanya kazi ndani yako hata kama huoni haimaanishi Mungu hafanyi.. umejitahidi kwa sehemu kubwa kutaka kubadilika katika eneo fulani lakini unaona kuna ugumu fulani Ndugu inashindikana kwa sababu unataka kutumia nguvu zako.
Wewe muamini Mungu na fanya kwa sehemu yako ikiwa ni kuomba,kusoma neno,kujiepusha na mambo mabaya mengine muachie Yeye.
Mfano halisi wa maisha yangu…
Nakumbuka nilipokuwa naanza shule kabisa darasa la kwanza takribani mwezi mzima kwenye somo la Hisabati siku ya kwanza tulikuwa tunaandika moja,moja,moja(mpaka ukurasa mzima unajaa na tulikuwa tunaanzia nje pia kuandika hizo moja moja chini) siku ya pili tunaandika mbili,mbili mpaka ukurasa mzima pia unajaa huku tunatamka.. siku ya tatu ilikuwa hivyo hivyo na siku zilizofata ukweli nilikasirika na kuanza kuona katika umri huo niliokuwa nao kwamba..
“Mbona hapa kama tunacheza tu? Ni nini sasa tunafanya hapa kila siku haya haya tu na sioni kitu chochote kimeongezeka ndani yangu .” Hivyo nilikuwa naona ni kama ujinga fulani na nilikuwa napoteza muda.
Lakini kumbe haikuwa hivyo ingali sikuwa naona kitu nakifanya lakini kumbe ubongo ulikuwa unafanya kazi ya kushika na kukalili na nikajikuta tu naweza kusema hii ni moja tena kwa uhakika hii ni mbili inaandikwa hivi. Nikajikuta naweza kujumlisha,kuzidisha nk kwa sababu tayari ubongo ulikuwa umeshaelewa vizuri juu ya kile nilichokuwa naona ni kazi ya kuchosha.
Hivyo ndugu haijalishi kabisa kwamba huoni mabadiliko yoyote kwa sasa lakini tafakari wewe wa sasa hivi 2025 ni sawa na wewe wa 2021 ulipokuwa katika wokovu ni wazi kuna hatua kubwa umepiga wakati mwingine bila hata kujua..
Kulikuwa na baadhi ya mambo unayafanya na ulikuwa unaona kawaida lakini saivi ukiyafanya unaona si sahihi na hata huwezi kuyafanya. Ni hatua hiyo umepiga..
Mtazame yeye wala usikate tamaa kabisa..
LWaebrania 12:2“tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.”
Alistahimili aibu(kusurubiwa uchi kabisa) hakujali kwa sababu ya upendo wake kwako na kwangu akakubali kuacha kila kitu.. mtafakari sana huyu mtu kama aliweza kufanya yote hayo anashindwaje kukubadilisha?
Je Yesu Kristo ni kipi kimewahi kumshinda? Amewahi kushindwa na kipi? Tafakari ni wapi Yesu Kristo alishindwa ukipata kuwa hakuna sehemu aliyoshindwa basi amini pia kwako hatashindwa kabisa..
Yeye ni asiyeshindwa kamwe ndio asili yake ilivyo mtumaini yeye..
Ikiwa una hangaika katika suala la utakatifu unaona ni mzingo,imani yako haipo sawa kama unamashaka,upendo wako si kama wa 1 Wakorintho 13:4-7 na unatamani kuwa kama hivyo unatamani tunda la Roho(Wagalatia 5:22-23) lakini unaona kuna ugumu..
Nataka ni kuhakikishie amini mchakato unaoendelea ndani yako na kwamba mambo yote iliyobeba biblia yaani ukombozi na baraka zote hawakuandikiwa malaika,wala wanyama nk lakini hivyo ni mahususi kwa ajiri yako kabisa wala usikate tamaa maana hayo yote ni yako na yatakuwa katika Jina la Yesu Kristo.
Amini neno lake ni kweli na ni hakika kabisa.. inuka, badilisha mtazamo wako kuanzia sasa amini Roho Mtakatifu yupo pamoja na wewe hivyo kazi yako wewe ni kuomba,kusoma neno na kutii kile Roho Mtakatifu anataka ufanye mengine muachie Yesu mwenyewe anajua kazi aliyoianza yeye ataitimiza wala usihofu kabisa hatakuachia njiani amini hili lazima akukamilishe amini neno hili.
Wafilipi 1:6“Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;”
Huna sababu ya kuona haiwezekani wakatu Kristo yupo ndani yako.
Mwandishi wa Zaburi anasema..
Zaburi 138:8 “Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.”
Ni kipi kinakufanya uone haiwezekani? Imani ni kukiri kwamba inawezekana. Je unamashaka na wasi wasi, huna uhakika na haya? Tambua hofu na mashaka vipo ndani yako ni wewe kufanya uamuzi kipi kishinde ndani yako.. ukichagua imani ndio ikae juu ya vyote itakuwa na usipofanya hivyo masha yatakuwa juu ya kila kitu..
Chagua imani iwe juu ya kila kitu umepewa uwezo huo. Nami ninakuombea katika Jina la Yesu Kristo Mungu akupe hekima ya kuelewa zaidi hili.
Ubarikiwe sana.
Mawasiliano:0613079530.
@Nuru ya Upendo.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.