Je! Baada ya kuokoka kuna kuomba maombi ya kujikomboa kwenye laana na vifungo?.
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima!
Je! Ni kweli baada ya mtu kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wake na kusamehewa dhambi zake mtu huyo anakuwa bado kuna laana za ukoo na familia na mababu zinamfata? Na anakuwa yupo katika vifungo mbali mbali ambavyo anatakiwa aombe sana ili azidi kujifungua na kujitoa katika vifungo hivyo alivyofungwa?.
Kipindi naokoka mwanzoni kabisa nikiwa na kama miezi miwili nilikutana na kitabu kimoja kimeandikwa “Maombi ya kujifungua katika vifungo vya kiza mbali mbali kwa siku 21″ kama sikosei kiliandikwa hivyo na nilipofungua ndani nilikuta mwongozo na nikaanza kuufata kwa kuomba yote wakati mwingine nakutana na maombi ya kujifungua kutoka katika bahari kuna majini nimeunganishwa nayo,kulikuwa na hayo maombi ya kukata Mawasiliano na majini bahari na kuzimu ilihari nimeokolewa.. nk
niliomba sana na hali yangu ilizidi na kuendelea kuwa mbaya sana kiroho nikawa mtu wa mashaka na wasisi na nikawa natumia nguvu kubwa sana kuomba lakini muda huo sifahamu kwa undani zaidi kazi ya Yesu Kristo nikawa nasumbuka sana na maombi huku sina ufahamu wa Yesu Kristo.. badala ya kuimarisha mahusiano yangu na Mungu nikajikuta najikita zaidi na kupambana na vitu ambavyo havikuwa vinanijenga..
ni mambo ambayo nimekutana nayo kwa Wakristo wengi nao walikuwa wanafahamu hivyo na kuamini hivyo na kuomba hivyo lakini leo tutajifunza ili kupata ufahamu bora zaidi..
Karibu
Ni jambo ambalo linaonekana kuchukuliwa kwa uzito na Wakristo wengi kuwa ni sawa na watu wanaamini hivyo na wengine wanafunga na kuomba maombi ya kujikomboa na kujitoa katika laana au vifungo vya kiukoo au familia..
Lakini je! Jambo hili ni kweli? Jibu ni la jambo hili si kweli hata kidogo pale tu mtu anapomwamini Yesu Kristo huyo mtu anakuwa amesamehewa dhambi zake zote(Mungu hatazikumbuka tena) lakini si hivyo tu..
Hata kama alikuwa ameingia katika maangano ya kiukoo,uchawi nk pale tu anapomwamini Yesu Kristo (siku ya kwanza kabisa) anakuwa ametolewa katika utumwa wa shetani na dhambi na utumwa wa kila namna anakuwa amehamishwa katika ulimwengu wa giza na kuletwa katika ulimwengu wa Nuru. Yesu Kristo anasema..
Yohana 5:24
“Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”
Unaona hapo anasema..! Yule alielisikia neno lake yaani injili na kuamini katika hiyo injili yaani kumwamini Yesu Kristo huyo mtu anaouzima wa milele ndani yake lakini haishii hapo tu huo uzima wa milele unakujaje anamalizia kwa kusema “Bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”
Swali la kujiuliza je! Mtu aliena uzima wa milele ndani yake yaani kaokolewa na kufutiwa deni ya dhambi yaani kapita kutoka mautini kwenda uzimani anavuka na vimelea vya mauti? Jibu ni la.
Lakini maandiko yanasema tena juu ya mtu huyu alieokoka kwamba…
1 Petro 2:9
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;”
Je sisi ambao ni mzao mteule,makuhani wa kifalme na taifa Takatifu na watu wa miliki ya Mungu je tunaweza kuwa na laana na kuhitaji kujifungua katika vifungo? Yaani unachukua muda mwingi kuomba kwamba najifungua katika vifungo vya kiukoo vya kifamilia, vya mababu na majini nk na wakati wewe ni mzao mteule,kuhani wa Kifalme na mtu wa miliki ya Mungu ambae ..
Hapo Zamani ulikuwa gizani(kabla hujaamini) na baada ya kuamini umeingia nuruni yaani hakuna tena laana wala vifungo ulivyonavyo wewe uko huru Haleluya!.
Warumi 8:31
“Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?”
Hivyo Mungu anapokuwa upende wetu yaani (ndani yetu kupitia Roho wake Mtakatifu) je ni nani aliye juu yetu? Jibu ni la hakuna laana wala vifungo juu yetu..
Sasa kwa nini inakuwa hivi na Wakristo wengi wanaamini hivi?
Hiyo ni kwa sababu ya kukosa maarifa ya kutosha kumhusu Yesu Kristo. Watu wamekosa kufahamu kwa undani kazi kubwa ambayo Kristo aliifanya pale msalabani mpaka akasema imekwisha. Maana yake alikamilisha kweli kweli.. Kristo anapomuokoa Mtu hamuachi na masaria au makando Kando anamuweka kuwa huru kweli kweli..
Mfahamu zaidi Yesu Kristo na kila siku tamani kumuelewa kwa viwango vingine. Na yeye atatembea na wewe na kukuonyesha mambo mengi sana na makubwa na atakufunulia mambo mengi sana sana. Ameahidi ukimuita yeye ataitika tu..
Yeremia 33:3
“Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu
usiyoyajua.”
Kinachokufanya uone kama bado kuna vitu vinakufunga ni ufahamu wako (akili yako) au fikra zako ndio zinakwambia kuna laana au vitu fulani vinakufatilia vya kiukoo nk na ukitoa nafasi ya kuanza kupambana navyo kufunga na kuomba ndio unavyompa nafasi shetani na ufahamu wako utageukia katika kuamini mambo hayo tu..
Badala ya kupambana na mambo hayo hebu pambana kuimarisha mahusiano yako vizuri na Mungu. Hakikisha unamfahamu sana Mungu kwa kusoma biblia,kuwa muombaji,kuwa mtu mwenye shauku ya kujifunza zaidi.. ufahamu wako utaanza kubadilika kabisa siku baada ya siku..
Jukumu lako kubwa pambana kuanza kubadilisha ufahamu wako na uelekee kwa Mungu na siku zote ikiwa umemuamini Kristo kuwa na mtazamo chanya siku zote(mtazamo wa ushindi na ndivyo ilivyo hakuna kushindwa katika Kristo Yesu na jambo lolote lile bali tunashinda zaidi ya kushinda Haleluya).
Yatafakari zaidi yaliyojuu utaanza kuona ufahamu wako unaelekea mambo yaliyojuu siku zote. Na hutakaa na kuanza kuona kuna mambo ya kiukoo yanakufatilia kamwe..
Wewe hakuna awezae kukutoa katika mkono wa Mungu wala kukutenganisha na Mungu labda uamue mwenyewe lakini nje na hapo hata aje nani hakuna awezae kukutenga na Mungu.
Warumi 8:35
“Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?”
Fikra zetu siku zote zinapingana na uharisia yaani mambo ya rohoni na tunatakiwa kuzibadilisha fahamu zetu.
Romans 12:2
[2]Do not be conformed to this world (this age), [fashioned after and adapted to its external, superficial customs], but be transformed (changed) *by the [entire] renewal of your mind [by its new ideals and its new attitude],* so that you may prove [for yourselves] what is the good and acceptable and perfect will of God, even the thing which is good and acceptable and perfect [in His sight for you].
Unaona hapo anasema “renewal of your Mind’ anafafanua zaidi na kusema katika mabano by its new ideals and its new attitude
Maana yake….
Warumi 12:2
[2] Wala msiifuatishe namna ya dunia hii (ya wakati huu), [kubadilishwa na kuzoea desturi zake za nje, za kijuujuu], bali mgeuzwe (mgeuzwe) kwa kufanywa upya [kabisa] nia zenu [kwa mawazo yake mapya na mtazamo wake mpya], ili mpate kujua [kwa ajili yenu wenyewe] ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayokubalika na ukamilifu, ambayo ni mema na yanayokubalika kwa Mungu, na kupendezwa na jambo lake.
Nia zenu maana nyingi ni akili zetu au ufahamu wetu ambao katika humo kuna mtazamo unaweza kuwa chanya au hasi.
Amini kabisa na ndio ilivyo kuna laana za ukoo wala za mababu wala chochote umekombolewa na imarisha zaidi mahusiano yako na Mungu kwa kutembea katika njia zake epukana na dhambi wala ibilisi usimpe nafasi kabisa..
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.