Amka utoke katika upofu wa Kiroho.
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Mtume Paulo anawaandikia watakatifu waliokuwa Thesalonike maneno haya..
1 Wathesalonike 5
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
Unaona hapo anasema. “… _Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe,na kuwa na kiasi .” Ikiwa na maana kuna uwezekano mkubwa wa Mkristo kulala usingizi yaani kuwa kama watu wa mataifa tu.
Na hiki kitu ndio anachokifanya Shetani katika kanisa la Mungu, Wakristo wengi sana wako usingizini. Wanatembea kama wana wa Usiku, wamelala.
Shetani amefanikiwa kuwapiga upofu wa rohoni Wakristo wengi maana yake amewapa kuona vizuri katika mambo ya ulimwengu lakini si katika mambo ya ufalme wa Mbinguni.
“ Leo hii mambo yanayowafurahisha watu wa ulimwengu huu ndio yanayowafurahisha na Wakristo pia.”
Yaani mambo yanayowapa furaha watu wa ulimwengu huu ndio yanawapa furaha watu wa Mungu jambo ambalo ni hatari mno.
Na kwa sababu wamepigwa upofu hata siku ya Bwana itakapofika hawatajua chochote ndio wale wanawali Watano Wapumbavu, atakapofika bwana harusi taa zao zitakuwa zimeshazima tayari na hawataweza kwenda kwenye karamu ya Mwana Kondoo ndugu kuwa makini sana
Kwa muda wako Soma Mathayo 25:1-13.
Ni muhimu kufahamu kuna mambo yanayoleta upofu katika maisha ya Mkristo na ukiyafahamu ni muhimu sana kuyaepuka hayo. Kwa sababu yatakufanya uendelee kulala katika usingizi wa Kiroho.
Tutazame nini maana ya usingizi wa Kiroho?Ni hali ya kutokujali/kuchukulia kawaida mambo ya rohoni. Ilihali tunasisitizwa kukesha, kuwa na kiasi,kuishi maisha ya utaua,kuomba.nk
Leo hii Wakristo wengi ni wazembe katika mambo ya kiroho yaani wamelala/wamepigwa upofu.
Mkristo Leo hii kwake aombe au asiombe kwake ni kawaida tu,asome neno au asisome anaona ni kawaida tu,aende kanisani au asiende kwake anaona ni kawaida tu,afanye dhambi asifanye dhambi kwake anaona ni kawaida tu, ahubiri asihubiri anaona ni kawaida tu nk.
Adui anachokifanya na anachopambana nacho hasa ni kukupofusha usione mambo ya rohoni na usipoona maana yake utayapuuzia hutaona yana uzito sana ndio maana mahubiri Mengi umesikia post ninyi kama hizi umesoma nk lakini hazina matokeo kwako kwa sababu unazichukulia kawaida tu. Mambo ya ulimwengu huu unayakumbuka kwa sababu huyachukulii kawaida.
Hata somo ulilofundishwa jumapili mbili za nyuma au moja ukiulizwa hukumbuki na unaona ni kawaida kabisa.
Ndugu amka usiendelee kulala muda umebakia mchache sana.
Mambo yanayoweza kukupofusha Kiroho ni haya na kama unayafanya yaache kuanzia leo hii. Chagua kukua na siku ile isikupate kama mwivi.
1.Miziki ya kidunia.
Hii ni injili ya Shetani na anayeitia mafuta ni Shetani mwenyewe kupitia waimbaji wanaoimba aidha hawajui au wanajua.
Sifa ni ibada kamili kabisa mtu anaeimba huyo mtu anafanya ibada katika roho kwa kujua au kwa kutokujua. Unapochukua muda wako kuisikiliza na kuiimba kitu inachofanya inakwenda kuziba ufahamu wako wa rohoni. Na kufanya usione mbele tena juu ya ufalme wa Mungu unatakiwa kuwa nani na kusudi lako ni nini na unatakiwa uishije utajikuta kuongea kwako kufikiri kwako nk ni nje na neno la Mungu kabisa.
Ikiwa iko kwenye simu yako futa haijalishi ni mizuri sana unaipenda ondosha utaelewa baadae ni nini ninachokisema..
Usiwe mtu wa kubadilika unatoka kusikiliza za kidunia unaenda unasikiliza nyimbo za injili usijidanganye kabisa acha.
Miziki ya kidunia hiyo haijatiwa mafuta na Roho Mtakatifu ili utakapoiimba umtukuze Mungu.
Huwezi kumtukuza Mungu katika miziki ya namna hiyo kuanzia kwenye fahamu zako mpaka kwenye moyo wako utakuwa unasifu kitu kingine kabisa.
2.Anasa za ulimwengu huu(Mpira,Tamthilia,).
Haya ni mambo yanayochukua nafasi katika moyo wa mtu, na ndio maana ni rahisi sana unapokuwa kanisani kuwaza ukitoka hapo ukamalizie Tamthilia yako, uwahi kwenye mpira, lakini huwazi ukitoka hapo ukayatendee kazi hayo uliyofundishwa. Huwazi naboresha vipi mahusiano yangu na Mungu, huwazi na kufikiri ufalme wa Mungu unaenea vipi katika ulimwengu huu,huwazi namna ya kutembea vizuri katika mapenzi ya Mungu.
Lakini asilimia kubwa unawaza hayo mambo tamthilia,Mipira,na unatumia nguvu kubwa ya Muda wako pamoja na Pesa zako na Sauti yako na akili zako katika kushangilia nk huwazi hiyo sauti yako inatakiwa itumike kuwaokoa watu wengine kwa njia ya injili, hiyo fedha ungeitoa sadaka kwa watumishi wa Mungu wanaohubiri injili(unakwenda kuitoa mpirani,kuweka tamthilia vinakujenga nini rohoni au hivyo vitu vinakusogeza karibu na Mungu tafakari) ikiwa ni mastendi,kwenye magari,mitandaoni ili iwawezeshe kupeleka injili mbele.
Hivyo wewe unakuwa ni mtu unaewaza duniani tu hapa, na unayachukulia kawaida tu mambo ya rohoni yaani kuchelewa ibadani kwako si kitu ni kawaida tu dada,mama,baba, usione ni kawaida.
Wekeza nguvu zako katika ufalme wa Mungu ndio hazina unayoweka mbinguni, muda wako unapoutumia vizuri kws Mungu unaweka hazina mbinguni nguvu zako nk.
Acha kufatilia Tamthilia, acha kushabikia mipira,usiyumbishwe na masumbufu ya mali,futa miziki ya kidunia kwenye simu yako nk wekeza Muda wako mwingi kwa Mungu na kila kitu chako utaanza kuona mambo ambayo hukuwahi kuyaona (Yeremia 33:3) utaanza kuuelewa ufalme wa Mungu ukoje,siri utaanza kufahamu na utajua tuna muda mchache wa Yesu Yupo karibu kurudi na utakuwa na uhakika wa kwenda naye.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano: 0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.