Swali: ni nani huyo anayetajwa katika Hesabu 24:17
Jibu tusome;
Hesabu 24:17 Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.
Huyo anayetajwa hapo, bila shaka ni YESU KRISTO Mkuu wa Uzima na Bwana wa Mabwana, yeye ndiye ile nyota ya asubuhi inayong’aa sana kama isemavyo maandiko.
Ufunuo wa Yohana 22:16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
Huyu ndiye aliyetabiriwa zamani, kwamba atakuja kuchunga Israeli kwa fimbo ya enzi, katika ule utawala wake wa miaka elfu hapa duniani, kumbuka sisi pia watu wa mataifa tuliompokee tunaingizwa katika ukoo wa Ibrahimu hivyo tunakuwa waisraeli wa rohoni.
Ufunuo 2:26-29 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
[27]naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.
[28]Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
[29]Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa..
Je! Umempokea ipasavyo? Au umempokea kwa jinsi ile ya kidini?
Yeye anasema..
Marko 8:34-38
[34]Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
[35]Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
[36]Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
[37]Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?
[38]Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
Je! Umejikana nafsi yako na kumfuata kweli kweli? Au bado unamchanganya na ulimwengu? Bado unamchanganya na ulevi, na uasherati, na uchafu?
Ikiwa, hujampokea ipasavyo, basi wakati ndio huu.. usiendelee kuchelewa maana wakati wowote atafunga mlango na mtu yoyote hatoweza tena kuingia.. hivyo jitahidi sana uingie kabla hujachelewa!!
Luka 13:24-25 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
[25]Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
Tubu dhambi zote na umaanishe kuziacha kabisa kisha tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na Kwa jina lake (KWA JINA YESU) ili upokee kipawa cha Roho Mtakatifu bure atakayekuwezesha kuishi maisha ya utakatifu siku zote.
Shalom.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.