Je unafahamu mtego wa manabii wa uongo.

Biblia kwa kina No Comments

 

Je unafahamu mtego wa manabii wa uongo.

Manabii wa uongo wanafanana na BUIBUI. Je unafahamu njia anayoitumia buibui kujipatia chakula?

Buibui ni mdudu ambaye huwa anatabia ya kujitengenezea utandu (mtego) kwa lengo la kunasa wadudu wengine wadogo wadogo kama nzi kwa ajili ya chakula.

Hivyo mdudu asiyekuwa na nguvu ya kupita kwenye huo mtego..huwa anakuwa chakula cha buibui.

Buibui amebeba ufunuo wa manabii wa uongo jinsi wanavyojipatia chakula chao (mali, fedha n.k) kutoka kwa wakristo wasio na nguvu ya kiroho (wakristo wa uongo) ambao wanafanana na wale wadudu kama nzi wasio na nguvu ya kupita huo mtego wa buibui.

Mtego wanaotumia manabii wa uongo ni pamoja na miujiza kadha wa kadha ambao mkristo asiyekuwa na nguvu za Roho Mtakatifu ni lazima tu anase kwenye huo mtego na hivyo kuwa chakula kwa huyo nabii wa uongo (buibui) kama vile nzi anasavyo kwenye ule mtego wa buibui kwa vile asivyokuwa na nguvu.

Hivyo ndugu jitathimini nguvu zako, je unaweza kukwepa huu mtego wa manabii wa uongo ambao wameongezeka sana katika hizi siku za mwisho, au umeshanaswa na kuwa chakula chao?

Ikiwa umeshanaswa na unahitaji msaada..basi unaweza ukatupigia, nasi tutakupa njia ya kutoka kwenye huo mtego.
Pia kama utahitaji kuwajua zaidi manabii wa uongo tutafute inbox tutakutumia masomo yanayohusu manabii wa uongo.

Ubarikiwe.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *