Nini maana ya kuhesabiwa haki kwa imani?

Biblia kwa kina No Comments

Nini maana ya kuhesabiwa haki kwa imani?

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Kama Wakristo ni Muhimu sana kuelewa jambo hili sio katika akili zetu tu basi likawa kama taarifa fulani tu ambayo tunaifahamu maandiko yanasema hivyo lakini jambo hili ni msingi dhabiti sana kwa Mkristo yeyote anaetaka kutembea katika maisha ya imani.

Huu ni kama msingi na mtu asipoelewa vyema hapa akawa na taarifa au kujua maandiko mengi yanayozungumzia kuhesabiwa haki kwa imani lakini asifahamu kwa kina na ndani ya Moyo wake basi hili ni eneo ambalo shetani atamtaabisha kwa sehemu kubwa.

Shetani anawataabisha Wakristo wengi na mawazo au hisia ambazo hazina uhalisia kabisa na Neno la Mungu. (na bahati mbaya wanaamini hisia zao kuliko Neno la Mungu ambalo ni kweli)

Leo hii Wakristo wengi shetani anawataabisha na mawazo kama haya..

“Mungu anakuchukia,Mungu hana mpango na wewe,Mungu hawezi akakukumbuka wewe, Mungu hapendezwi na wewe tabia yako ni mbaya, Mungu akuangalie mtu kama wewe una nini? Huna faida yoyote mbele za Mungu nk”

Ili hali uhalisia wa maandiko na ukweli unasema hivi..

Isaya 49

15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.16 Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

Mungu amesema hatakusahau kamwe lakini kwa sababu ya kushindwa kuelewa haya Wakristo tunakaa na kua na huzuni kama watu tuliosahaurika kabisa.

Sasa basi nini maana ya kuhesabiwa haki?

Ni kitendo cha Mungu mwenyewe kumfanya mtu kuwa mwema(mwenye haki au mwenendo mwema) ikiwa na maana Mungu anamfanya mwenye dhambi kuwa hana hatia, yaani kuwa sawa na yeye kwa njia ya imani kupitia Yesu Kristo. Kazi ya ukombozi aliyoifanya Yesu Kristo pale msalabani.

Mungu mwenyewe kwa maamuzi yake pasipo kusukumwa wala kushawishiwa na kitu chochote anakuondolea makosa yako yote ambayo kupitia hayo ilikupasa hukumu lakini yeye anakuhesabia haki kwa njia ya imani kupitia Yesu Kristo.

Mungu hatazami matendo yetu ili kutuhesabia haki mbele zake haki hii ni kwa njia ya imani katika Yesu Kristo sio  kwa matendo yetu maana kwa njia ya matendo yetu hakuna mwenye haki mbele za Mungu.

Sasa watu wengine wenye nia ya kupotosha kweli wataanza kusema unapotia bidii katika imani kwa kufanya matendo yanayompendeza Mungu kujiepusha na uovu watakwambia hayo ni matendo ya sheria(utasikia unapambania wokovu kwa matendo) lakini kuna tofauti. Yapo matendo ya sheria na yapo Matendo ya imani( _yaani imani inaambatana na matendo kama maandiko yanaposema aaminiye na kubatizwa. Maana yake mtu anapoamini tendo linaloendana na hiyo imani yake ni ubatizo Sasa hatuwezi kuita ubatizo ni matendo ya sheria bali ni tendo la imani)._

Hivyo  hakuna mwanadamu yoyote asiyekuwa na hatia amabe ni msafi na anastahili kuhesabiwa haki kwa sababu ya Matendo yake kuwa yeye ni  msafi, hayupo isipokuwa Yesu Kristo peke yake.

Maandiko yanasema..

Warumi 3:23” kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;”

Hivyo jukumu kubwa tulilonalo ni sisi akili zetu,Fahamu zatu na mioyo yetu kuhakikisha inakubaliana na hili jambo tusifatishe na kukubali mawazo yanayokuja katika fahamu zetu, bali tulazimishe akili zetu zikubaliane na ukweli tunaouona kwenye maandiko na si kukalili na kujua kuelezea vizuri lakini ndani yetu hatuna uhalisia huo tunaona bado hatustahili.

Haki inatupa kustahili ambapo hatukustahili hivyo unapokosa na ukaanza kusikia hukumu ndani yako kuwa hufai,Mungu hatakusamehe,hustahili, wewe ni mchafu nk kataa kili maandiko yamesema..

Yohana 1
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Kiri wewe ni mtoto wa Mungu, wewe ni mwenye haki, Mtakatifu na mteule wa Mungu katika hali ya udhaifu unaojiona nao unapoanza kukiri hivyo kila siku kukataa mawazo negative ndani yako ndipo utakapoanza kuona uhalisia wa wewe ni nani na adui hatakutaabisha kabisa.

Warumi 5:1
“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,”

Kuwa na Amani, hofu inatoka wapi? Mashaka yanatoka wapi ikiwa..
Mungu amechagua kukupenda,kukuhesabia haki na ndivyo maandiko yanavyosema hakuna anaeweza kwenda kumshawishi asikuhesabie haki,asu aukuchukie hakuna anaeweza. Wala matendo yako hayawezi kumfanya Mungu aghaili kukupenda. Maana upendo wake ni mkuu kuliko dhambi zako.

Wajibu ni wako Sasa kuchagua kuamini Neno la Mungu linasema nini juu yako au kuamini uongo unaotokana na shetani kupitia fikra zako.

Nakuombea katika jina la Yesu Kristo nguvu na neema ya kuliamini neno na sio kuamini hisia zako.

Ubarikiwe sana.
@Nuru ya upendo.
Contact:0613079530.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *