
MBIGILI NI NINI?
Mbigili ni aina ya mmea inayotambaa ardhini na ambayo matunda yake yana miiba kali inayoweza kuumiza miguu na mikono ikishikwa, Maumivu yake huwa ni makali sana. Tazama picha hapo juu.
Katika biblia Neno hili limetajwa katika vifungu mbali mbali.
Isaya 5:5-7 “Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa;
[6]nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, BALI LITAMEA MBIGILI na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
[7]Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio”.
Soma tena..
Isaya 7:23-24 Tena itakuwa katika siku hiyo kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu, iliyopata fedha elfu, patakuwa mahali pa MBIGILI na miiba tu.
[24]Mtu atakayekwenda huko atakwenda na mishale na upinde; kwa sababu nchi yote itakuwa ina mibigili na miiba.
Hosea 10:8 “Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.”
Soma pia Mika 7:4 utaona neno hilo.
Mbigili inafunua nini katika roho?
Kibiblia, miiba, huwakilisha “mahali palipolaaniwa”. Hivyo mmea huu wenye miiba mikali sana inafunua laana ya Mungu itakayowakuta watu wake watakapomuacha.
Adamu alipoasi, Mungu alimwambia ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, hivyo itatoa miiba na michongoma. Na matokeo yake ni kwamba italimwa kwa shida.
Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Ndio maana shamba ambalo halipaliliwi au halitunzwi, matokeo yake ni kuwa linatoa miiba, ikiwemo mbigili.
Mithali 24:30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. 31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. 32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. 33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Na vivyo hivyo na sisi tuliokolewa kwa neema ni shamba la Mungu.
Isaya 5:7 “Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli…”
Hivyo yatupasa tujihadhari sana tusimuache Bwana, maana itakuwa tumejitakia laana kwake ambayo ni maumivu makali yasiyoelezeka yatatupata, ni kutengwa na uso wa Bwana milele kama Kaini na Yuda Isikariote.
Jihadhari na uasherati, uzinzi, uongo, usengenyaji, uvaaji mbaya, tamaa za kidunia na mambo yote mabaya.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.