Waepuke Wanaojiita Wakristo wa namna hii.

Biblia kwa kina No Comments

Waepuke Wanaojiita Wakristo wa namna hii.

Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

Katika nyakati za mwisho hizi yapo makundi ya watu wanaojiita Wakristo lakini maisha yao yanatofauti kabisa wala hayaendani hata kidogo na Ukristo. Tofauti na ilivyozoeleka kwa watu kuwa ukristo au wakristo ni dini lakini ukweli ni kwamba ukristo ni Zaidi ya dini yaani ukristo ni maisha. Ukristo ni maisha ambayo mtu anayaishi ndani na nje ni Zaidi ya dini ukisoma katika maandiko sehemu pekee ambapo watu waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza ni wale waliokuwa kule Antiokia.

Matendo 11:26” hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.”

Mwanzoni walikua wanaitwa wanafunzi, au wale wa njia lakini kadili walivyozidi kukaa Zaidi katika kujifunza na jinsi mwenendo au maisha ya wale watu, watu wa nje waliona hawa ni watu ambao wanafanana na Kristo kwa sababu maisha yao yalikuwa yalibadilishwa kuanzia ndani mpaka nje.

 

sasa wapo watu wanaojiita Wakristo lakini ukweli ni kwamba maisha yao hayaendani wala kufanania kabisa na watu wana namna kama hii epukana nao kwa namna yoyote ile maana ni rahisi sana ukikaa nao kukuambukiza tabia zao na mwisho ukajikuta unaiacha ile kweli. Na watu hawa wameandikwa wapo katika maandiko. Sasa tutasoma kitabu cha 1 Wakorintho tutaona hawa ni watu wa namna gani.

 

1 Wakorintho 5:10-11 “Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

 

 

[11] Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.”

Ukisoma huo mstari wa 11 Paulo anasema msichangamane na mtu aitwaye “NDUGU” kwa kiingereza anasema “who claims to be a beliver” yaani yeye ambae anasema na kukiri kuwa ni mwamini lakini huyo mtu bado  ni mzinzi,muabudu sanamu, mlevi, nk

Muabudu sanamu anazungumziwa hapa sio mkatoliki la! Bali ni mtu ambae anasema amemuamini Yesu Kristo lakini kilicho na nafasi kubwa moyoni mwake sio Kristo bali ni mambo mengine kama vile kazi,Elimu,Mume,mke familia watoto, anasa za ulimwengu huu ikiwa ni mipira maana yake yupo tayari kumpoteza Kristo kulicho hicho kitu cha thamani anachokiona yeye maishani mwake. Huyo ni mtu anaeabudu sanamu.

Wapo Wakristo wanaosema tumeokolewa na tuna uhuru katika Yesu Kristo chochote unaweza kufanya wala huwezi kupoteza uzima wa milele wala Mungu hawezi kukuchukia na Mungu ataendelea kukutumia na kama ni huduma inaendelea tu. Lakini sivyo hivyo kabisa watu wa namna hii waepuke sana kabisa nitakuonyesha ni kwa namna gani hawa watu walivyo.

“Tunamuamini Yesu Kristo na uchafu wetu wote lakini hatuendelei kubakia vilevile kazi ya msalaba ni kuu mno”

1 Wakorintho 6:12” Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.”

 

Maandiko yanasema vitu vyote ni halali kwetu lakini mwandishi sio vyote vifaavyo maana yake japokuwa vyote ni halali kwako vipo ambavyo vinamadhara kwako na kama ukivifanya lazima utaangamia. Na ndio maana anasema kuwa sitatiwa chini ya kitu chochote maana yake ukitiwa chini ya hicho kitu means umekua mtumwa wa hicho kitu.Ukisoma chini anaendelea kusema……….

1 Wakorintho 6:13” Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwi”

 

Maandiko yanaweka wazi mwili si kwa zinaa bali ni kwa ajili ya Bwana ni hekalu la Bwana.

Hivyo wapo wanaojiita Wakristo na hawakemewi na wachungaji wao kwa kuwaogopa kwa sababu wanawaletea zawadi wanatoa michango mingi kusapoti ujenzi wa kanisa au kununua vitu au kupeleka injili mbele wanaogopa kuwakemea au kuwatenga ili kuwasaidia hali zao za kiroho

Watu wa namna hii usichangamane nao kabisa maana hawana ukristo wowote ndani yao waepuke unaona mtu ni rafki yako lakini yuko bize na mambo ya ulimwengu sana kuliko Mungu yuko tayari kutokwenda maombi nk kwa ajili ya mambo yake yeye havutiwi sana na mambo ya kiroho bali ya mwilini tu ndugu epukana na mtu wa namna hi kabisa.

Ubarikiwe sana.

@nuru ya upendo.

Contacts 0613079530

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *