FAHAMU HATUA AMBAYO SHETANI ANATAKA UIFIKIE.

Biblia kwa kina No Comments

FAHAMU HATUA AMBAYO SHETANI ANATAKA UIFIKIE.

shalom nakusalimu katika jina la Yesu Kristo, karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu.

Shetani kuna mahali ambapo anataka kila mtu aliemwamini Yesu Kristo aifikie hatua Fulani na mtu huyo akishafikia katika hatua hiyo basi kwake shetani ni ushindi mkubwa sana maana kwa mtu huyo ni ngumu sana kurudi na ndio maandiko yanasema.

2 Wakorintho 2:11 “11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.”

unaona hapo anasema “shetani asipate kutushinda” maana yake kuna uwezekano wa shetani kutushinda kama tusipojua hila zake.

Shetani kitu anachokifanya shetani kwa sasa hapigani vita vya yeye kutaka kushinda haraka la! Anachokifanya shetani anapigana vita vya taratibu sana lakini vyenye matokeo makubwa sana kwa baadae. Vita anavyopigana shetani na waamini wengi kwa sasa ni kuhakikisha anawanyong’osha na kuhakikisha wanafikia hatua ya wao kunyoosha mikono kwamba haiwezekani.

Sasa hivi shetani haji kukwambia huwezi,utashindwa la anachokifanya anahakikisha anatengeneza mazingira ya wewe mwenyewe kusema hili jambo haliwezekani ingali maandiko yamesema inawezekana.

Na katika eneo moja wapo kubwa ambalo shetani anapigana na waamini ni katika eneo la utakatifu. Mtu anaanza kutembea na Mungu kwa viwango vya juu Zaidi ikiwa ata maintain kuishi maisha matakatifu.

sasa ni kwa namna gani shetani anapigana vita hivi? Lengo la shetani sio kwamba anafurahia unapoanguka na kuamka ndio anapata ushindi shetani hapati ushindi wowote unapoanguka katika dhambi kwa sababu anajua kabisa unaweza kuanguka na ukaamka tena kama vile maandiko yanavyosema….

Mithali 24:16 “Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.”

Unaona hapo mwenye haki huanguka mara saba na hata akainuka tena, maana yake kuna uwezekano wa mtu anaeanguka katika dhmabi na akaamka tena akatembea na Mungu kwa viwango vya juu sana ikiwa mtu huyo atatubu kwa kudhamiria kabisa na kuchukua hatua stahiki za kuondoka katika hali hiyo.

sasa shetani jambo analolifanya mtu anapoanguka dhambini huenda leo mtu amezini akatubu na kudhamiria kwamba hatafanya hivyo maana ndivyo inavyokuaga kwa kila mtu sasa anachokifanya shetani ni kuendelea kukutengenezea mazingira yaw ewe kuendelea kuanguka au kurudia hicho kitendo.

Shetani atatumia nguvu kubwa kuhakikisha anakurudisha tena katika jambo hilo hilo na ndio hapo unakaa tena baadaya miezi miwili inapita hujazini unaona umepona mwezi watatu unaingia kuna vishawishi vya hali ya juu sana kukutaka wewe urudi tena kuzini utakataa sana kwa ndani utapigana lakini utaona kama huwezi kuvumilia unajikuta unarudi tena kufanya kitendo kama hicho tena unaanguka tena.

Unakataa tena baada hata ya miezi sita unarudi kuzini tena wewe utakuwa wakati mwingine ni mtu wa kutafakari sana kwa nini inakua hivyo? Utajitahidi kutafakari sana ila unaweza usipate jibu. Utajitahidi kufunga na kuomba lakini inaweza isisaidie kitu.

Bado shetani ataendelea kukutengenezea mazingira kila baada ya miezi kama sita au mwaka unajikuta unaanguka tena katika zinaa.

Sasa hatua mabayo shetani anataka ufikie ni hii uone kwamba hilo jambo haliwezekani kabisa kuishi maisha matakatifu na utana kilamtu anaigiza tu hakuna lolote nae anazini tu vivyo hivyo sasa ukishafikia katika hatua kama hii ndipo ushindi mkubwa wa shetani unapoonekana.

Ukishafikia katika hatua hii kwanza hutaweza kuamini kitu kinaitwa utakafu, utaona wote wanaofundisha utakatifu ni wanafiki waongo,nk

Na hatua inayofata utaanza kutengeneza fundisho lako linaloegemea katika uchafu na kuanza utaanza kuitumia neema ya Mungu kwa kuhalalisha uovu kwamba unaweza kuishi vyovyote Mungu amekuchagua umeshaokolewa umeokolewa milele huwezi kupoteza wokovu.

Wahuburi wengi unaowaona mafundisho yao wanaona dhambi si kitu ni kitu cha kawaida tu jua kabisa shetani kashawaweza wala usitege sikio kuwasikiliza tayari kuna mentality ambayo shetani akashawafunga nayo na hawawezi kutoka huko unless kwa neema ya Bwana Yes utu lakini nje na hapo haiwezekani.

Jambo ambalo natamani uendelee kulishikilia hata kama unaanguka mara kwa mara katika uzinzi,wiz ink endelea kuamini kwamba unaweza kuishi maisha matakatifu katika kizazi hiki cha ukaidi na uzinzi amini inawezekana endelea kusimamia katika msimamo huo peke yake utaona mwisho wasiku kwa kuendelea kusimama na msimamo huo itafikia hatua utaweza kusimama na hutaona unaanguka anguka tena.

Usikubali kukiri kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako haiwezekani kataa kabisa utauna mkono wa Bwana ninakuombea katika jina la Yesu Kristo hutashindwa na adui. Ni Imani yangu somo hili limekupa kusimama na kuona kwa sehemu hila za adui.

Mungu akubariki sana.

@Nuru ya upendo wa Kristo

contact: 0613079530

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *