Mawaa ni kasoro au dosari yoyote inayofanya kitu fulani kipoteze sifa yake iliyo nzuri. Kwa mfano mtu mwenye uso mzuri akipata jipu kwenye shavu tutasema ana mawaa kwa sababu lile jipu limeharibu uso wake… Au mtu aliyenunua bati kwa ajili ya kuezekea nyumba yake lakini bati lile likawa limetoboka hapo tunasema lina mawaa. Lakini pia ..
Author : magdalena kessy
Neno hili tunapoliona katika maandiko lina maana mojawapo kati ya hizi tatu, 1.Kushiba kiasi cha kutotaka tena kile ulichokipokea awali 2.Kuwadharau watu wengine na kuwafanyia mambo ambayo hupaswi kuyafanya 3.Kujigamba /kujiinua na kudhani wewe unajitosheleza mwenyewe Vifungu vifuatavyo limetumika kwa maana ya kushiba.. Mithali 25:17[17]Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; ..
JIBU.. Kuhadaa ni kudanganya yaani kutumia njia ya uongo/ ya mkato ili kiufanikisha jambo fulani… Tunalipata neno hili Katika vifungu hivi, Mwanzo 31:20 “Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia” Mithali 12:5 “Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa” Warumi 1:28 Na kama walivyokataa kuwa na ..
Tusome… Mwanzo 37:6 “akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake”. ..
Pitia hapa.. Ezekieli 27:8 “Wakaao Sidoni na Arvadi ndio waliovuta makasia yako; wana wako wenye akili, Ee Tiro, walikuwa ndani yako, ndio WALIOKUWA RUBANI ZAKE”. Marubani tunaowasoma hapo hawakuendesha ndege kama marubani wa sasa hivi kwa sababu kwa wakati huo ndege hazikuwepo. Neno rubani asili yake ni mwana maji na sio mwana anga kama linavyotumika ..
Tusome hapa.. Mathayo 14:23 “Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. 24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; MAANA UPEPO ULIKUWA WA MBISHO. 25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. 26 ..
Shalom, karibu tujifunze biblia, JIBUMwivi na mwizi ni neno moja lenye maana ileile ila ni lugha mbili ambazo zipo katika nyakati mbili tofauti. Biblia imetafsiriwa kwa kiswahili cha zamani kilichoitwa ‘kimvita’ ambacho kina maneno yasiyokuwepo kwa sasa kama vile mwivi na wevi yakimaanisha mwizi na wezi. Hiyo ndiyo sababu hatuwezi kuona neno mwizi na badala ..
JIBU.. Katika maandiko tunaona Yohana mbatizaji alibatiza kwa maji lakini alishuhudia kuwa Bwana Yesu atakuja kubatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto, Tuangalie sifa kuu tatu za moto.. Sifa ya kwanza ni :kuunguza na kuteketeza vitu visivyofaa kama vile takataka. Hapa ni pale Mungu anapozichoma dhambi zote zilizo ndani ya mtu na ndipo mtu anafikia ..
Kuna dhambi ambayo huleta mauti, mkristo akiifanya dhambi hiyo wakati ambao bado ana neema ya Mungu atakufa lakini siku ya mwisho atapata wokovu. Mfano Musa alipomkosea Mungu alisamehewa lakini hakuondolewa adhabu ya kifo…Mungu alimwambia kutokana na lile kosa hataiona nchi ya ahadi na hakika atakufa lakini alipokufa aliungana na watakatifu na kuna wakati alitokea na ..
Karibu tujifunze biblia.. Yakobo 3:1“Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.” Ukipeleka katika lugha ya kiingereza ” Not many of you should become teachers ..” au unaweza kusema ” pasiwepo na waalimu wengi kati yenu” Roho Mtakatifu anamvuvia yakobo kuyasema haya yanayolitafuna sana kanisa, Hii huonekana pindi Kila mtu anapokuwa ..