Choyo ni kitendo cha mtu kuwa na tamaa kubwa, mfano tamaa ya mali, uongozi, au chakula, na hii mara nyingi huambatana na ubinafsi, yaani umimi na kutumia vitu Kwa pupa ilimradi tu kumyima au kuwanyima watu wengine wasipate.
Mithali 21:26 “Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa; Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi”.
Tabia hii si nzuri wala ndani yake Haina faida yoyote zaidi tu ya kupata hasara na kupoteza uaminifu kwa na upendo kwa watu.. ndiyo maana Bwana Yesu alituonya tuepuke tabia hii maana tabia hii mfano wa kudiliki kutaka vyote kuwa vyako ili wengine wasipate kabisa ni jambo mbaya wala halipaswi kuwepo sehemu yeyoye mfano katika familia, utumishi, kazi na maneno yote jambo hili ni baya sana
maandiko yanatuonya
tusome
Luka 12:13 “Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.
14 Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?
15 Akawaambia, ANGALIENI, JILINDENI NA CHOYO, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu”.
Lazima tuwe makini na tabia hii kwa kuondoa ubinafsi wa namna yeyote katika maisha yetu
Tuwe watu wa kupenda kujali wengine kwa kupenda kuona wenye uhitaji wa kitu wanakipata/ kupenda haki kwa kumpa mwingine kile anachostahili kupewa kwa moyo safi na dhamiri njema.
Maana hata Upendo wa Mungu hakuwa wa kibinafsi alimtoa Yesu Kristo ili awe fidia ya wengi na Leo hii tunashuhudia badiliko kubwa katika maisha yetu,.Sasa na sisi kwa jinsi alivyotupenda, yatupasa j
kuwa yeye maana yeye ndiye kielelezo Cha maisha yetu hivyo nasi hatuna budi kuachana na tabia hiii na kukaa katika kupendana na kujariana bila upendeleo wowote
Yakobo 2
8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.
9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.