DHAMBI YA KUTOLIPA MADENI INAVYOWEZA KUMPELEKA MTU MOTONI
Kumekuwa na tabia ya wana wa Mungu wengi kukopa pasipo kulipa madeni wanayodaiwa, wengine hudhani ya kwamba wanapotubu tu Mungu anawasamehe madeni ya watu, HAPANA huko ni kujidanganya na kukosa maarifa, mtu anapotubu Mungu anamsamehe yale madeni anayodaiwa na Mungu mwenyewe tu nayo ni madeni ya dhambi lakini yale madeni ya watu yanabakia palepale na hayafutiki mpaka mwenyewe aamue kusamehe au alipwe pesa yake,
Wengine wanatabia moja ambayo inamchukiza sana Mungu, mtu anaweza kupata pesa na akaenda kuitoa sadaka kanisani na wakati huo huo huku pembeni kuna mtu anamdai, hilo ni kosa kubwa, inatupasa kukumbuka maneno ya Bwana wetu Yesu aliposema ”kama una neno na nduguyo usitoe sadaka nenda kwanza kapatane na nduguyo ndipo utoe sadaka yako” MATHAYO 5:24.
Kama umepata pesa ya watu inayotosha kulipa deni la watu huruhusiwi kuitoa sadaka mpaka ukamwambie mdeni wako naye akuruhusu lakini akikataa na kusema naitaka pesa yangu basi usiitoe bali umlipe pesa yake, kwasabu sadaka inapoletwa madhabahuni moja kwa moja Mungu anapoipokea anachunguza mioyo ya watu dhidi ya mtoaji je hakuna moyo unamshitaki mtoaji huyu? na endapo itapatikana moyo mmoja tu wenye neno juu ya mtoaji basi sadaka hiyo Mungu haipokei, sasa niafadhali tu ungeilipa deni la watu kuliko kuipoteza madhabahuni pasipo kuleta faida yoyote. ndiyo maana Mungu akasema anayekopa anakuwa ni mtumwa wa yule anayekopesha
Mithali 22:7 ”Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.”
Maana yake ni kwamba ukimkopa mtu au mtu akiwa anakudai kitu chochote mbadala kwa sababu yoyote ile unafanyika kuwa mtumwa wa mtu huyo.
MTU ASIYELIPA MADENI HUHESABIKA KUWA HAJAOKOKA
Mtu mwenye tabia ya kukopakopa pasipo kulipa, huyo anahesabika kuwa ni mfuasi wa Ibilisi, Mungu hana tabia hiyo, hivyo hata mtoto wake hawezi kuwa na tabia kama hiyo ya kukopa kopa pasipo kulipa.
Zaburi 37:21 Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hikirimu.
Biblia inasema hapa ASIYE HAKI yani ni mtu asiyemjua Mungu kabisa ni mtu wa mataifa mpagani HUKOPA WALA HALIPI, angalia maneno haya hajasema tu hukopa hapana ila hukopa wala halipi kwa maana kukopa siyo dhambi na hakumwondolei mtu haki hake kwa Mungu, bali kutokulipa ndiyo dhambi na inamwondolea mtu haki yake kwa Mungu, umeona hii mwana wa Mungu ili kujua kwamba kweli unahofu ya Mungu, nilazima utalipa deni lakini endapo hutalipa unahesabika kuwa ni mpagani wa kawaida tu.
Wakristo wengi wamenaswa na mtego huu wa shetani kwa kendekeza dhambi hii ya kukopa pasipo kulipa kwa kisingizio cha “upendwa” eti ni mpendwa hatanipeleka polisi ndio anaweza asikupeleke polisi na akakupeleka Jehanam ni afadhali akupeleke polisi ufungwe deni liishe kuliko akuache huru huku bado anakudai ni mbaya sana, Mtume Paulo alitambua vema kwa habari ya dhambi hii ya kutolipa madeni ya watu, hata siku alipokutana na Onesmo ambaye alimkimbia Bwana wake (Filemoni) kwa kosa fulani labda la wizi, Paulo alimshuhudia Onesmo hatimaye Onesmo akaokoka na baada ya hapo akamwandikia waraka aupeleke kule kule kwa bosi wake ambye ni Filemoni na pia kumlipia madeni yote anayodaiwa.
Filemoni 1:18-19 Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike hicho juu yangu. Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakuwia hata nafasi yako.
Ndugu yangu, ni heri ukauza ulivyo navyo ili kulipa madeni ya watu… kama vitu ni bora kuliko mbingu haya endelea kukaa navyo. Hakikisha leo unaanza harakati ya kulipa madeni yote unayodaiwa.. hata kama mdeni wako amesahau mkumbushe na mlipe, Kumbuka tunaposema madeni hatulengi tu yale unayodaiwa na watu wanaokujua, HAPANA, hata yale ya mtandaoni.
Unadeni la songesha, mpawa, Halopesa, Nipige tafu, n.k maadamu ulikopa ukatumia na hukurudisha..yamkini umesahau au ulitupa hiyo laini yenye madeni, nataka nikuambie hiyo dhambi inaweza ikawa sababu ya wewe kukosa mbingu kama hutolipa hayo madeni, ni heri ukalipa kidogo kidogo hadi umalize yote.
Bwana anataka tuwe wakamilifu..tusiwe na lawama yoyote katika ile siku ya hukumu.
Mathayo 5:48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Je! umeokoka kweli kweli?
Unahabari kuwa tunaishi ukingoni kabisa mwa siku za mwisho na mlango wa neema utafungwa muda wowote? Ikiwa hujampokea Yesu.. unasubiri nini mpaka wakati huu?
Hebu leo tubu dhambi zako zote na umaanishe kuziacha kabisa.. kisha tafuta ubatizo sahihi ili uwe miongoni mwa wateule wa Mungu.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.