Elewa maana ya zaburi 48:14, yeye ndiye atakayetuongoza.

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU, tusome..

14]Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.

Mwandishi anaanza kwa kumsifia Mungu wetu kwamba ni tabia yake siku zote kuwaongoza watu wake.


Anamaanisha kwamba Mungu hatamuacha mtu bali atamuongoza siku zote katika njia nzuri iendayo uzimani, njia nzuri ya kupigana vita, yenye kujenga na hata kupanda.

Ndivyo alivyofanya kwa wana wa Israeli walipokuwa jangwani alitumia wingu na nguzo ya moto kuwaongoza siku zote, aliwalinda kwa malaika wake, aliwafundisha njia za kupata faida katika kazi zao, aliinua waamuzi, manabii na wafalme ili kuwachunga, haya yote yanaonyesha dhamira yake ya kuongoza watu wake.


Na sisi bado tunaongozwa na yeye wakati huu hadi hapo tutakapokufa. Yesu alipotaka kuondoka alisema hatuachi kama yatima akatupa roho mtakatifu ili atuongoze na kututia katika kweli yote.

Yohana 16:13
[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

     Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *