Kwanini walemavu walizuiliwa wasimtumikie Mungu madhabahini pake

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na libarikiwe. Karibu tujifunze Maneno ya Uzima.

Tusome..
Mambo ya Walawi 21:16-24;
[16]Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

[17]Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

[18]Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,

[19]au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,

[20]au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;

[21]mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

[22]Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.

[23]Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.

[24]Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.”

Swali: Sasa ikiwa Mungu ni wa wote na hana Upendeleo kwanini Akataze WALEMAVU madhabahuni pake?

Jibu: Mambo mengi katika Agano la kale yalikuwa kivuli cha agano jipya yaani hayakuwa halisi bali kivuli cha yanayokuja (Waebrania 10:1,3:5, kolosai 2:17);

Ilikuwa ni ya mambo ya mwilini mfano sikukuu ya pentekoste ilikuwa sikuuu ya kukusanya mavuno kwa ajili ya Bwana Mashambani, lakini katika agano jipya sikukuu ya pentekoste waliookoka watu 3,000 kama mavuno ya Roho za watu badala ya mazao. Kumbe tunajifunza Agano la kale lilihusisha mambo ya kudhihirishwa mwilini ili kufundisha yale ya kiroho yanayokuja Baadae. Lakini haukuwa mpango wa Mungu yachukuliwe vilevile katika Majira yote, La!

Mfano halisi huwezi kumpa mwanafunzi wa darasa la tatu hajibu maswali ya form six ikiwa Bado hatua hizo bado hajazifikia  kiuhalisi hawezi kujibu maana Bado hajafikia hatua ile, lakini ukimpa maswali kulingana na hatua aliyo nayo haiwezi kumpa shida maana anao uwezo wa kuyajibu maana tayari alishafundishwa.

Vivyo hivyo na sisi Tulipokuwa tukifundishwa makusudi makamlifu Ya Mungu tulifananishwa na watoto wadogo (galatia4:1-6); Mungu angemleta Yesu Kristo asulubiwe, Afe amwage damu yake kwa dhambi zetu ndipo Tusamehewe bila kuwepo Agano la kale kabla, basi Tusingemuelewa vyema.
Hivyo Agano la kale lilileta taswira ya mambo ya mwilini /ya nje kwanza, Kisha baadae aitumie hiyo kuelezea mambo ya Rohoni.

Mfano Waliambiwa Wasile nguruwe kwasababu Hacheui, Yaani hawezi kurejesha chakula kukitafuna na kukimeza tena baada ya kule (kama Ng’ombe), lakini si kwamba Nguruwe ni mbaya sana bali ni kwa lengo sisi tusiwe na tabia hiyo ya kutocheua kiroho. Maana yake kama huwezi kutafakari uliyofundishwa au kutendewa na Mungu hapo kabla basi wewe ni najisi, maana hutakuwa na shukrani Wala Imani.

Wana wa Israel walifanya hili walipokuwa Jangwani walimuonyeshea Mungu manung’uniko wakisema umetuleta huku kutuua! Wasikumbuke Miujiza mikubwa waliyotendewa hapo nyuma kidogo tu.

Lakini Daudi alikabiliana na Goliati hakuogopa bali alisema yule Bwana aliyeniokoa na simba na dubu ataniponya Leo dhidi ya mfilisti huyu asiyetahiriwa. Maana yake Kiroho ni kwamba Daudi alicheua, lakini Wana Israel hawakucheua hivyo wakawa Najisi.

Turudi suala la madhabauni kama swali letu, Waliopewa nafasi kuhudumu hekaluni walikuwa makuhani pekee, tena uzao wa Lawi, nao endapo mzao wa Lawi akiwa na kilema chochote hakuruhusiwa kuhudumu hekaluni. Hata kabila lingine ikiwa si lawi; hawakuruhusiwa kuhudumu hekaluni haijalishi ni nabii au mtu gani hata wanawake hawakuruhusiwa walichukuliwa kama walemavu pia. Hivyo hawakutengwa walemavu pekee Bali na makundi mengine yote!

Angalia, Hapa tunafunuliwa kuwa Mungu alikuwa akionesha jinsi mtumishi wa madhabahu yake anapaswa awe, yaani Ukamilifu wa Rohoni! Asiwe mtu mwenye mapungufu. Hili ndilo kusudi kuu la Mungu na Wala si Upendeleo Wala walemavu kuchukiwa. ndio maana tunaona Yesu Kristo aliketi pamoja na walemavu (Marko 14:3) hata Leo tunaona Mungu wetu anaponya wagonjwa, viwete, vipofu n.k
Mungu wetu hashughuliki na ulemavu wa Mwilini Bali wa Rohoni ambao ndio Unajisi.

Wapo walemavu ambao Mungu mwenyewe ameacha wawe walemavu kwa ajili ya ushuhuda wake, nao wanamtumikia sana wanafanya miujiza wanaponya watu, na kuwafungua sasa utajiuliza kwanini asiwaponye na wao?
Mawazo ya Mungu hayachunguziki; Elia alikufa na ugonjwa wake lakini Mifupa Yake ilifufua wafu.

Tunajifunza, wakati wa sasa mbele za Mungu hakuna kilema Wala Mwanamke Wala mtumwa; Bali wote ni makuhani wake. Tumestahilishwa na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, Sasa tunaweza kuingia patakatifu pa patakatifu.

Pendo lake kwetu ni kuu sana! Jina lake na libarikiwe Milele.
Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *