Kitabu cha mithali kimeandikwa na nani?

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Swali: nani aliyeandika kitabu Cha Mithali?

Jibu: “.. SULEMANI, MWANA WA DAUDI..” Maneno haya tunayapata Mwanzo kabisa wa kitabu hiki, Mwandishi akijitaja mwenyewe kuwa ni Sulemani

Soma..

Mithali 1:1 “Mithali za SULEMANI, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu”

Neno Mithali, kwa kawaida linamaanisha “Msemo mfupi uliotungwa kwa ustadi, uliobeba aina fulani ya hekima.”

Lakini katika biblia kitabu Cha Mithali ni mkusanyiko wa hekima na kanuni, Maonyo, Maagizo ya Kiroho, Maarifa pamoja na mafunzo katika Maisha ya kawaida na vitu vya asili.

Katika utangulizi, Mwandishi anatuasa kwamba tutapata hekima au kuongeza zaidi Tuliyokuwa nayo, Baada ya kusoma kitabu hiki. Hivyo Kitabu cha Mithali ni kwa Kila mtu.

Inakadiriwa kitabu cha Mithali kiliandikwa miaka miaka mia tisa (900) kabla ya Kristo {K.K}.

MIGAWANYO YAKE:

Mithali 1-22:16, Hapa aliandika Mwenyewe Mfalme Sulemani.

Lakini tukianzia 22:17-24:34 hujulikana kama kitabu Cha tatu, Hizi ziliandikwa na Wengine lakini alizikusanya mwenyewe Sulemani.

Kuanzia Mithali 25-29 Biblia inaonesha Aliandika Sulemani, lakini zilirekodiwa na Watu wa Mfalme Hezekia.

Mithali 30; Hujulikana kama kitabu Cha Tano. Ambacho kiliandikwa nae Aguri Bin Yake.

Tukimalizia na sehemu ya Mwisho yaani Mithali 31; Hapa iliandikwa nae Mfalme Lemueli.

Lakini kuna mitazamo ya baadhi ya wanazuoni, wengine husema Aguri Bin Yake na Lemueli ni majina Mengine ya Sulemani. Kwa vyovyote lakini Kiliandikwa na Sulemani kwa sehemu kubwa, Na ndio maana huitwa kitabu Cha Sulemani.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *