fahamu maana ya dhabihu za roho kibiblia.

Maswali ya Biblia No Comments

Dhabibu za roho ni zipi, zinazotajwa kwenye biblia?

1Petro 2:5  “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo”.

Dhabihu ni sadaka za kuteketezwa hizi zilitolewa katika agano la kale. Hizi sadaka zilikuwa na lengo la kufanya upatanisho wa makosa ya watu, kwa mfano alipochinjwa mwanakondoo, au ng’ombe au mbuzi, au njiwa (Walawi 1:3-16) na kuteketezwa kisha ule moshi wake ukapanda juu basi huo ndio unakuwa uthibitisho wa sadaka yake kukubaliwa. Na mtu huyo dhambi zake zinakuwa zime funikwa kwa muda. Yaani zinakuwa hazijaondolewa baada ya muda kunakuwa na kumbukumbu la dhambi wakati mwingine kila mwaka.

Lakini kwenye hili agano jipya pia ipo dhabihu yetu, ambayo kwa kupitia hiyo tunapokea upatanisho wa dhambi na makosa yetu, na dhabihu yenyewe ni YESU KRISTO Bwana wetu ambaye yeye kama vile mwanakondoo alichinjwa kwa ajili yetu ili sisi tupokee wokovu na ondoleo la dhambi, hivyo yeyote ambaye yupo sasa ndani ya Kristo Yesu tayari ameshamtolea Mungu dhabihu ya upatanisho wake.

Ila tunapokuwa ndani ya Kristo yesu, tuna haja ya kuonyesha kuwa tumekombolewa na yeye, kwa matendo yetu. Hivyo ni lazima tutaonyesha tabia kama za mtu anayekwenda kutoa dhabihu mbele za Bwana, na sio kama za mtu aliyejiamulia tu. Na tabia zenyewe ndio hizo zinazojulikana  kama dhabihu za roho ambazo sisi tunazitoa.

1) Shukrani

Zaburi 50:14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.

Zaburi 69
30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani.

Hivyo ukiwa mtu wa shukrani kwa Mungu, Ni kudhiilisha kuwa umejua kazi ya msalaba wa kristo ndani yako. Na hizi shukrani ni lazima ziwe katika Sifa za kinywa chako, pamoja na matoleo kwa kile Mungu alichokubariki. Ni lazima ufahamu sana wewe kama mkristo kuwa mtu wa shukrani muda wote, Wote walio kwenda kupeleka sadaka za namna hii mioyo yao ilijaa shukrani kwa Mungu wao, hawa kwenda mikono mitupu.

2) Moyo uliopondeka

Zaburi 51:16 Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. 

17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

Moyo uliopondeka ni moyo wa toba(Geuko), wa majuto ya dhambi, ambao unakufanya ukose raha moyoni mwako kwasababu ya makosa yaliyofanyika, na hivyo unakupelekea ujishushe sana mbele za Mungu.

Mtu mwenye moyo huu, mbele za Mungu anaonekana kama amejiona yeye ni mkosaji, na hivyo Yesu amefanyika upatanisho kwa ajili yake, tofauti na mtu yule ambaye vitu vyote kwake ni sawa, hata baada ya kuona kosa bado anaufubaisha moyo wake, kujifanya kama haja kosa chochote mbele za Mungu. Yatupasa wakati wote tuwe watu wa kujishusha mbele za Mungu. Watu wa kupenda rehema zake.

Unapojitunza nakuweka mbali mambo ya kidunia, kisha ukaufanya utumike kwa ajili ya kazi ya Mungu, hapo ni sawa na unamtolea Mungu sadaka yenye maana sana, yaani unaenda mbele zake Mungu na badiliko, unasema msalaba mbele, dunia nyuma. Lakini ukiwa unavaa ovyo ovyo, unazini,unaiba unatumia mikorogo, unajichora mwili wako, unakunywa pombe, unavuta sigara, unatoa mimba, hapo hufanyi ibada yoyote mbele za Mungu. Kwasababu lazima ufahamu kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu (1Wakorintho 3:16).

Hivyo, wewe ambaye umeokoka, zangatia mambo hayo matatu, SHUKRANI, MOYO ULIOPONDEKA, NA KUUTOA MWILI WAKO. Wokovu wako utakuwa na maana sana mbele za Mungu.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *