Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Tupende kukupa tahadhari Mtu wa Mungu dhidi ya upotovu na mafundisho ya kuhusu tafsiri za ndoto. Ukikosa tafsiri sahihi za ndoto zako kimaandiko, wengi wamejikuta wakijitenga na imani na kuanza kuziangalia ndoto zao kama dira ya maisha yao kama ilivyotabiriwa na mtume Paulo (soma 1 timothy 4:1)
Awali ya yote kabisa inabidi tufahamu ndoto zimegawanyika katika makundi makuu matatu..
1. NDOTO ZINAZOTOKANA NA MUNGU
Hizi huja na ujumbe, tahadhari Fulani zinazolenga kukurekebisha pale unapokosea, utende HAKI au ukaze mwendo katika kumtafuta Mungu n.k. Mfano tunajifunza kwa habari ya mke wa pilato katika biblia
Mathayo 27:19 ” Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika NDOTO kwa ajili yake.”
2. NDOTO ZINAZOTOKANA NA SHETANI
Hizi zinaambatana na vitisho, Hofu, Tamaa ya kutenda dhambi, na mambo kama hayo ya kukutenga na Mungu. Mfano kuota unazini na watu unaowajua au usiowajua, kuota unafanya matambiko, ngoma za kimila n.k hizi huletwa na Adui mwenyewe, Sasa mtu anapaswa azikemee, na arekebishe mwenendo wake ikiwa ni pamoja na kumpa Kristo maisha.
3. NDOTO ZINAZOTOKANA NA MTU MWENYEWE AU MAWAZO
Mfano kazi yake, Chakula alichokula au anachokipenda, mazingira yanayomzunguka n.k. Na hizi ndizo hutawala sana Ulimwengu wa ndoto (95%)
Ndoto Katika kundi hili hazipaswi kupewa uzito wowote aidha kama hayo makundi mawili yaliyoelezwa juu. Bali zinapaswa zipuuzwe maana hazibebi Ujumbe wowote. Bali ni marudio ya yale yalioujaza ufahamu wa mtu husika katika Ulimwengu wa ndoto yaani Shughuli, watu wa karibu, mazingira yanayomzunguka n.k Mfano Mtu anaona Ajali mchana na usiku anaota ajali nyingi zinatokea, mchana unakuwa msibani usiku unaota mtu mwingine kafa mpo kweny mazishi, au Mtu ni dereva anaota Anaendesha gari usiku n.k
Hivyo unapoota ndoto za namna hii usitafute tafsiri zake maana hazitoki kwa Mungu Wala Shetani Bali ni katika ufahamu wako. Kama Maandiko yanavyosema
Mhubiri 5:3 “Kwa maana NDOTO huja kwa sababu ya SHUGHULI nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.”
Aina nyingine ya ndoto zinazotokana na Mtu ni zile za Kula. Biblia inasema..
Isaya 29:8 “Tena itakuwa kama MTU mwenye NJAA AOTAPO, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.”
Unaona, kumbe ukilala na njaa usiku kuota unakula chakula ni jambo la kawaida tu, mfano kuota unakula nyama, karanga, wali , samaki, matunda, mayai au keki. Au unaweza kuota unakula na haushibi zote hizo zinaweza kutokana na ulilala bila kula Jana au umekula vyakula hivyo kwa siku za karibuni au umekuwa ukivitamani. Hivyo ukiota hizi Uzipuuzie! Endelea na mambo mengine, Soma sana neno la Mungu maana ndilo linaloweza kukutabiria maisha ya mbeleni ipasavyo.
Maana ndoto na maono vyote SI kitu mbele ya neno la Mungu, zinafananishwa na makapi. Tusome..
Yeremia 23:28-29
28 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana.
29 Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?”
Sikiliza Mpendwa, PENDA sana kujifunza neno la Mungu kuliko kujifunza tafsiri za ndoto, JE! SI ni kama kulinganisha ngano na makapi yake?( Ndoto na neno la Mungu)Jifunze neno na Mungu atakuwa Pamoja na wewe.
Ikiwa bado hujaokoka basi mlango wa Neema u wazi bado, na ukifungwa hautafunguliwa Tena basi okoka Leo! Tubu dhambi zako angali upo hai( hakuna Toba kaburini) kumbuka tunaishi katika nyakati za nyongeza tu Yesu yupo mlangoni kurudi kwa ajili ya kanisa lake. Mgeukie Leo na Mungu atakubariki sana
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.