Fahamu mahali pa juu panapozungumziwa kwenye biblia ni wapi? (1 Samweli 9:12)

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo Lihimidiwe. Karibu kujifunza Maandiko_ 

“Mahali pa juu ” Hapa ni mahali palipoinuka ambapo watu walitengeneza madhabahu na kutoa dhabihu zao . Palikuwa ni popote penye mwinuko au mlima, Hii ilifanyika kuwa ni Heshima kwa Mungu kumfanyia madhabahu mahali palipoinuka kuashiria kuwa yeye yu juu ya yote..

Mtu wa kwanza kufanya madhabahu mahali pa juu au palipoinuka ni “Ibrahim”. Napo ni mlima Moria ambapo alitengeneza madhabahu kwa ajili ya kumtoa Isaka mwanawe.

Kwa mifano zaidi kuhusu mahali pa juu..

1 Samweli 9:11-12

11 “Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko?

12 Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu WATU WANA DHABIHU LEO KATIKA MAHALI PA JUU;”

pia hata mfalme Sulemani alikuwa akitoa dhabihu mahali pa juu

(Mlima Moria) Kabla ya kujenga hekalu hapo..

1 Wafalme 3:2-3

2 Ila watu walikuwa WAKICHINJA DHABIHU katika MAHALI PA JUU, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la Bwana, hata siku zile.

3 Sulemani naye akampenda Bwana, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika MAHALI PA JUU .”

Pia kwa vifungu zaidi kuhusu mahali pa juu 1 Nyakati 16:39 na 1 Nyakati 21:29

Lakini pia walikuwepo waliojifanyia madhabahu mahali pa juu kwa ajili ya miungu yao, na kuitolea dhabihu miungu hiyo jambo ambalo likawa chukizo sana mbele za Mungu!

 1 Wafalme 14:22-23 

22 “Basi Yuda wakafanya maovu machoni pa Bwana; wakamtia wivu, kwa makosa yao waliyoyakosa, kuliko yote waliyoyafanya baba zao.

23 Maana hao pia wakajijengea MAHALI PA JUU, na nguzo, na maashera, juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi.”

Jambo kama Hilo utaliona pia 2 Wafalme 16::4, 17:9-11,29_

Sasa swali ni JE? Mahali pa juu ambapo leo tunaweza mtengenezea Mungu wetu madhabahu inayompa Heshima ni wapi?

Yohana 4:19-24

19″ Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!

20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.

21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

23 LAKINI SAA INAKUJA, NAYO SASA IPO, AMBAYO WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. KWA MAANA BABA AWATAFUTA WATU KAMA HAO WAMWABUDU.

24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” 

kumbe mahali petu palipoinuka Leo si milimani, Wala penye miinuko bali katika Roho zetu , Na huko ndiko madhabahu za Mungu zinatengenezwa.

JE mpendwa Rohoni mwako ni madhabahu ya Mungu? au ya miungu? Na hii haijalishi unaabudu au kutoa sadaka kiasi gani lakini rohoni mwako hakuna madhabahu ya Mungu, Basi fahamu fika ya kuwa unaitumikia miungu ya kigeni. Kama moyoni mwako kuna uasherati, Ulevi, masengenyo, uchawi, wizi n.k basi wewe ni Najisi mbele za Bwana Mungu wako.

 Mathayo 15:19

Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

Bwana atusaidie tumjengee madhabahu sahihi Rohoni mwetu

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *