Fahamu Mambo yanayoweza kukughalimu katika Ukristo wako

Biblia kwa kina No Comments

Fahamu Mambo yanayoweza kukughalimu katika Ukristo wako.

nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

Yapo mambo mengi katika safari ya Imani kama usipoyafahamu yatakughalimu kwa sehemu kubwa na safari ya Imani hutaifurahia kabisa kwa sababu hutakuwa na Amani na mwisho wa siku utaona kama Mungu hana mpango na wewe kabisa na unaweza ukarudi nyuma ukakata tamaa, ukajikuta unaishia njiani na kwa bahati mbaya sana shetani yuko makini na utendaji wake wa kazi hivyo inatupasa kuwa makini kwa sababu adui yetu yupo macho usiku na mchana akitafuta njia ya kuturudisha nyuma, ashukuliwe Mungu atupae kusimama na kushinda na Zaidi ya kushinda.

tutaangalia mambo yasiyopungua manne ambayo kama tukiyaacha yaendelee kuwa ndani yetu basi safari ya Imani itakuwa nzito.

1. Ujinga
Ujinga sio tusi bali ni kutokufahamu/kujua kitu, mtu yeyote asiyefahamu kitu Fulani basi huyo mtu ni mjinga katika hicho kitu lakini akijifunza anaweza kuelewa na asiendelee kuwa mjinga kwenye hicho kitu.

Wakristo wengi yapo mambo mengi hawayajui na ni ya Muhimu kwao ya rohoni lakini ajabu ni kwamba hawataki kujua yaani kujifunza na matokeo yake wanaendelea kuwa hivyo hivyo na matokeo yake maisha yao ya kiimani yanaishia kuwa ni magumu.

Ujinga ni gharama, usipojua kitu hujui utabakia kuwa hujui kama hutataka kujifunza, usipojua utaingia kwenye changamoto kwa kutokujua. Na shetani anapata nafasi katika maisha ya Wakristo wengi kwa sababu ya kutokujua kwao.

Maandiko yanasema….

Hosea 4:6 “Watu wangu *wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;* kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”

Unaona hapo hasemi “ _watu wangu wanaangamia…._ ” Anasema “’…Watu wangu WANAANGAMIZWA..” maana yake kuna kinachowaangamiza kwa sababu ya wao kukosa maarifa kwa sababu kwanza walichukia maarifa yaani hawakutaka kujua. Na ndio maana wakajikuta wanaingia katika shida.

maandiko tena yanasema

Isaya 5:13” Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.”

Unaona sabababu ya hawa watu sabababu ya kuchukuliwa mateka ni nini ni kwa sababu ya kukosa kuwa na maarifa.
Maarifa yanayozungumziwa hapa sio ya shule bali Ujinga wa kiroho (kutomjua Mungu na mapenzi yake) huleta utumwa, mateso, na kupotea hata  kama mtu anaonekana yuko sawa nje.

Leo hii wakristo wanafikiri watapata tu maarifa ya kumjua Mungu na wataweza kumshinda shetani huku wako busy na kuangalia tamthilia na anasa za aina zote wanawekeza sana katika mambo yasiyokua na faida katika roho zao kushinda katika page mbalimbali ambazo mwisho wa siku hazina maudhui ya ki-Mungu wako busy na siasa,mipira,tamthilia nk sisemi mtu asifatilie kujua hata hali ya nchi inaendaje lakini unapata muda wa kujifunza Zaidi ni mambo mambo mangapi huyajui na unaendelea kukaa hivyo tu?.

2.Uvivu 

Wakristo wengi wanadhani mambo ya kiroho huwa yanakuja tu automatically katika kipindi Fulani pasipokujua kama vile ukisema ukae tu usifanye kazi basi ipo siku tu pesa zitakuja na utakua ni tajiri, kama mwilini haiko hivi unategemea vipi rohoni iwe hivyo? Mkristo anaona kufungua kusoma kitabu ambacho kimebeba hatima na mwongozo wa maisha yake yaani biblia.

Wakristo wengi wanaona uvivu hata kuifanya kazi ya Mungu wanasema muda ukifika huenda watafanya kazi ya Mungu haina Muda maalumu kufika anza kufanya acha visingizio kumbuka kuna vitu huwezi kuvipata kanisani au sehemu nyingine yeyote isipokua katika kuhubiri njili.
Kadili unavyosema nitasoma kesho/nitajifunza kesho ndio muda unavyozidi kwenda mwisho a siku utajikuta huwezi kabisa hiki ni kitu kitakughalimu kwa sabababu mafanikio ya kiroho na kimwili sio kwa ajili ya watu wavivu bali ni kwa ajili ya watu ambao wameamua kuweka uvivu pembeni

Mithali 13:4 “Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.”

Mithali 6:9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaamka lini katika usingizi wako?”

3.Kupuuzia
Wakristo wengi kuna mambo tunajua ni ya muhimu kuyafanya lakini tunayapuuzia na kuona ni kawaida tu. Kana kwamba tuyafanya hata tusiyafanye tunaona ni kawaida maandiko yanaonya kuhusu dhambi,kuhusu shetani lakini tunaona ni kawaida tu wala hatuweki umakini katika hayo. Wakristo wengi wanajua maombi ni muhimu,kusoma neno ni Muhimu lakini watu wanafanya kwa kujisikia hii ni hatari mno kwa sababu ni mwanya ambao adui ndio anautumia kuleta mambo mabovu katika maisha ya Wakristo.

Wakristo wengi huwa wanaona ni kama stori tu zinazozungumzwa lakini hawajui kama ni uhalisia. Mpaka wanapoingia katika changamoto Fulani ndio wanajua kuwa kumbe ni halisi na haya ni mambo ambayo yanagharimu watakatifu wengi.

Yapo mengi lakini yatafakari haya machache na yafanyie kazi na mafunuo mengine ambayo Mungu atakupa na kukumbusha usiyachukulie kawaida fanyia kazi, na nimekuombea neema ya Bwana Yesu ikuwezeshe na upate kuwa imara Zaidi mampando ya adui yaondoke.

Ubarikiwe sana.
@Nuru ya upendo
Mawasiliano: 0613079530

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *