Hosana ni nini kama tunavyosoma Katika Maaandiko?

Uncategorized No Comments

Hosana, neno la Kiyahudi linalomaanisha “OKOA,” lilionekana likitajwa mara ya kwanza siku Ile alipokuwa anaingia Yerusalemu.

Yohana 12: 12 “Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;
13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, HOSANA! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!”
Habari hiyo hiyo inapatikana kwenye vifungu hivi Mathayo 21:9, Mathayo 21:15, na Marko 11:9-10.

Kwanini watumie Neno la Hosana yaani “okoa”, badala ya labda “karibu” au “tuponye”

Ikumbukwe kuwa Waisraeli, waliokuwa chini ya utawala wa Waroma, na walikuwa wakitazamia kwa hamu kuja kwa Masihi ili kuwaokoa kutoka katika utumwa na maadui.

Wengine walimwamini Yesu kuwa ndiye Masihi, wakibeba matawi ya mitende na wakishangilia alipokuwa akiingia Yerusalemu. Na kwasababu walikuwa wanayajua maandiko kwamba ipo siku Masihi (yaani Kristo), atakuja na kuwaokoa na utumwa wote na maadui zote..kama maandiko yanavyosema…katika Zekaria
Zekaria 14: 3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita”.

Wanafunzi wa Kiyahudi pia walitazamia kwa hamu wakati ambapo Masihi angewapigania na kuwarudishia ufalme. Baada ya Yesu kufufuka, walimuuliza kama alikuwa anarudisha ufalme kwa Israeli. Yesu alijibu kwamba haikuwa kazi yake kujua nyakati au majira, bali kwamba wangepokea nguvu Roho Mtakatifu atakapowashukia. Kisha akawaagiza wawe mashahidi katika Yerusalemu, Yudea, Samaria, na katika dunia yote.

Matendo 1:6 “Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?
7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao”.

Wakati wa wokovu mkuu kwa Israeli haukuwa wakati Masihi aliporudisha ufalme. Badala yake, walipaswa kuhubiri injili kwa mataifa yote kwanza. Injili ilipohubiriwa na watu kuokolewa, Kristo angeshuka kutoka mbinguni kwa nguvu nyingi na kuwapigania Israeli. Huu ungekuwa mwanzo wa utawala wa miaka 1000 wa Yesu Kristo duniani, ambapo angetawala kwa amani na kutawala kutoka Yerusalemu pamoja na watakatifu wake.

Hivyo utafika wakati ambapo Kristo atashuka kutoka mbinguni kwa nguvu nyingi, naye atawapigania Israeli na kuwaokoa, wakati huo injili itakuwa imeshamalizika kuhubiriwa kwa mataifa yote na unyakuo utakuwa umeshapita, na ndio utakuwa mwanzo wa utawala wa Miaka 1000 ya Yesu Kristo hapa duniani, ambapo utakuwa utawala wa Amani, na atatawala akiwa pale Yerusalemu, Israeli Pamoja na watakatifu wake aliowanyakua.

Ubarikiwe

Jiunge pia na Channel yetu ya  WhatsApp. 

“ NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Masomo mengine:

Kibanzi na Boriti kwenye biblia vinamaanisha nini?

Je kujichua/ kufanya punyeto (masturbation) ni dhambi?

Arabuni maana yake ni nini? ( Waefeso 1:14)<< KANISA NI NINI? na je linaundwa na nani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *