Ielewe sadaka ya moyo katika maandiko.

Maswali ya Biblia No Comments

 

Je sadaka ya moyo ipoje?

Tusome,

Walawi 22:21 “Na mtu awaye yote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au SADAKA YA MOYO WA KUPENDA, katika ng’ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema ndani yake cho chote”.

Sadaka ya moyo wa kupenda ni sadaka iliyotolewa na wana wa Israel bila kuagizwa wala kupewa sharti lolote, walitoa kwa kupenda wenyewe..

Wakati huo kulikuwa na sadaka walizotoa kwa sababu maalumu mfano sadaka ya shukrani ilitolewa kwa lengo la kumshukuru Mungu baada ya kufanyiwa jambo fulani. Lakini sadaka ya moyo wa kupenda ilitolewa bila sababu yoyote ile, hawakuagizwa lakini walitoa kwa sababu wao wenyewe walipenda kufanya hivyo.

Mfano wa sadaka hiyo ni pale wana wa Israeli walipotoa sadaka zao ili kujenga Maskani ya Bwana. Mungu hakuwa amewaagiza kufanya hivyo lakini wao wenyewe waliguswa kutoa wakamwambia Musa dhamira yao na kisha wakaanza kuleta sadaka zao.

 

Kutoka 35:29 “Wana wa Israeli WAKALETA SADAKA ZA KUMPA BWANA KWA MOYO WA KUPENDA; wote, waume kwa wake, AMBAO MIOYO YAO ILIWAFANYA KUWA WAPENDA KULETA KWA HIYO KAZI, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa”.

Kutoka 35:21 “Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu”..

Soma tena Kutoka 25:2 na 2Nyakati 29:31.

Je katika agano jipya bado tunazo sadaka za namna hii?

Ndio sadaka hizi bado zipo na tunatakiwa kuzitoa kwa sababu sadaka kama hizi zinapendeza mbele za Bwana. Katika agano jipya tunaona jambo hili katika andiko hili..

2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu”.

Unaona hapo sadaka ya moyo wa kupenda ni sadaka inayompendeza na kukubaliwa na Mungu sana..

Je unapomtolea Mungu huwa unatoa kwa moyo wa kupenda au unatoa kwa sababu ya shinikizo fulani? Siku zote usiache kumtolea Mungu lakini hakikisha unatoa kwa moyo wa kupenda maana hapo ndipo utakapompendeza Mungu..

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *