IMEANDIKWA.
Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari meneno ya uzima.
Ukisoma katika kitabu cha Mathayo ile sura ya nne wakati Yesu anajaribiwa kule jangwani na ibilisi utaona katika kila eneo shetani alipokua akimjaribu Bwana Yesu Bwana Yesu katika sehemu Zote anajibu “IMEANDIKWA“
Watu wengi huwa tunalitumia hili Neno kwa namna ya kawaida tu, na ndio maana tunatamka Neno la Mungu imeandikwa hivi lakini bado tunaanguka kwenye makosa ya Neno hilo hilo ambalo tumelitamka..
Maana halisi ya kusema “ imeandikwa “ inamaanisha kusimama na hilo Neno, maana yake unaliamini,unalielewa na hakuna kitu chochote kinachoweza kukutoa katika hicho unachokiamini ndani ya moyo wako juu ya hilo Neno ndani ya moyo wako.
Imeandikwa maana yake ni kusimama na hilo Neno katika nyakati zote unatembea nalo bila kuangalia uhalisia au mazingira yanayokuzunguka yanasemaje kwa wakati huo..
Hivyo Bwana Yesu alivyokua anasema imeandikwa ni zaidi ya tunavyofikiri kwamba alikua na torati tu kichwani la! Bali ni kitu ambacho Bwana Yesu alikua anakielewa na kusimama nacho..
“ Huwezi ukasimama na kitu ambacho huna uhakika nacho., yaani Huwezi kusimama na Neno ambalo huna uhakika nalo” Yesu Kristo atusaidie sana.
Hivyo inahitaji Neno lifunuliwe ndani ya Moyo wako na Roho Mtakatifu uone uhalisia wa hilo Neno( kuona uhai wa Neno la Mungu ndani yako, maana yake Neno la Mungu linatakiwa liwe hai katika moyo wako/ndani yako na likiwa hai ndani yako utajua tu.)
Neno linapokua hai ndani yako ndio utakua na uhakika na kusimama nalo haijalishi ni nini kitakuja mbele yako mtumishi wa Mungu hutaweza kuliacha Neno (Muombe Mungu akupe Neno la Kusimama nalo katika hali yoyote ile )
Tuangalie Mfano mmoja hapa kwa undani kidogo ambao alijaribiwa Bwana Yesu.
Mathayo 4
8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
Hili linaweza kuonekana ni jaribu la kawaida lakini lilikua ni jaribu zito ambalo nimetamani kulifatilia na kwa sehemu ufahamu nimeshindwa kuelezea.. yaani sina maneno ya kuelezea kama ipasavyo.
Ili tupate ufahamu mpana tusome biblia Amplified kisha nitaweka tafasiri..
Matthew 4:8-9
[8]Again, the devil took Him up on a very high mountain andKisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, showed Him *all the kingdoms of the world and the glory (the splendor, magnificence, preeminence, and excellence) of them* .
[9]And he said to Him, These things, all taken together, I will give You, if You will prostrate Yourself before me and do homage and worship me.
Maana yake…
Mathayo 4:8-9
[8] Tena, Ibilisi akamchukua akampeleka juu ya mlima mrefu sana, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wake (yaani fahari, uzuri wake wa kuvutia, ukuu wake, na ubora wake wa hali ya juu).[9] Akamwambia, Mambo haya yote kwa ujumla wake nitakupa, ikiwa utajinyenyekeza chini (utaanguka kifudifudi) mbele yangu na kunitolea heshima pamoja na kuniabudu.
Unaona hapo mstari wa nane? Anasema akamuonyesha falme zote źa ulimwengu na utukufu wake yaani Fahari ya huu ulimwengu(Mungu kaiumba dunia na fahari ya isiyokua ya kawaida ni vile ufahamu wetu hatujafamu kumbuka ulimwengu huu ni mbingu ambayo alipewa mtu kuishi, anasema uzuri wa kuvutia..
Kumbe dunia hii haina uzuri tu bali inao wa kuvutia, si hivyo tu ina ukuu wake maana hii ni mbingu ambayo alipewa Adam kuishi sisi ambao ni copi ya Mungu sio hivyo tu ina ubora wake wa hali ya juu sana)
Vitu ambavyo alionyeshwa Bwana Yesu mimi na wewe hatujawahi kuviona kabisa(Umeshawahi kuona falme zote za ulimwengu)..
Nikwambie jambo kama hujasimama na Mungu vyema shetani akikuonyesha hivi vitu akakwambia maneno yale aliyomwambia Bwana Yesu utamwambudu kama “IMEANDIKWA” hujasimama vyema.
Kristo hakufanya hivyo kwa sababu alisimama na Neno je unapokua katika majaribu unalikumbuka hata Neno la Mungu linasema nini juu ya jambo hilo?
Yesu alijua shetani vyote anavyomuonyesha ni vya wizi na vyote Mungu anaweza kumpa (wafili 2:5-10)na zaidi ya hivyo alivyoonyeshwa na adui kwa kujua ukweli huu na zaidi ya hapo akasimama asiweze kuyumba usifikiri kwamba Yesu alikua havitaki kumbuka alikua mwandamu kama mimi na wewe 100% tufanye bidii sana sana Neno la Mungu liwe halisi ndani ya mioyo yetu, tusiwe watu tunapita kwenye majaribu tunaelewa nini juu ya hali tunayoipitia?.
Tia bidii kukesha kwa ajili ya kuomba Bwana Yesu usimama imara katika wito wako Neno la Kristo liwe hai ndani yako katika kila hali.
Mungu akubariki sana
Mawasiliano:0613079530
@Nuru ya upendo.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.