Je maombi ya toharani yapo kibiblia?

Maswali ya Biblia No Comments

 

JIBU,

Watu wengi wamekuwa na imani hii kwamba kuna uwezakano wa kumtoa mtu kuzimu (kwenye mateso) kwa kumuombea, jambo ambalo halina ukweli wowote kulingana na maandiko, kwasababu kama hilo linawezekana basi pia kuna uwezakano wa kumtoa mwenye haki kwenye paradiso,

Kama jambo hilo la kumtoa mwenye haki paradiso haliwezekani basi fahamu kabisa na maombi ya kumtoa mwenye dhambi kwenye mateso pia hayapo kabisa,

Tusome..

Luka 16: 22 “ Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, KATI YETU SISI NA NINYI KUMEWEKWA SHIMO KUBWA, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu”

Ukisoma mstari wa 26, anasema, sisi na ninyi KUMEWEKWA SHIMO KUBWA, ikiwa ina maana mtu hawezi kuvuka kutoka huku aende kule na wa kule aje huku, kwasababu Katikakati yetu kuna shimo kubwa,ikiwa kitendo cha kuvuka tu hakiwezekani itakuwaje maombi ndio yawezekane, kuomba kwako hakuwezi kumtoa kabisa..

hakuna wakati mwingine utakaokufanya utengeneze maisha yako zaidi ni ukiwa hapa duniani, unayo nafasi ya kuyaweka maisha yako Katika njia nzuri, kwa kuwa hakuna nafasi nyingine utakayopata ukifa,kule kuzimu kunaeleza hali ya maisha yako uliyoyaishi duniani, maana yake ulishindwa kujua hatma yako baada ya kufa unataka kwenda wapi?,

ikiwa tuna mifano ya watumishi wa Mungu waliosimama na Mungu Katika ukamilifu wote lakini walishindwa kuwatoa watu kuzimu itakuwaje mimi na wewe ndugu tunaotenda dhambi, Ibrahimu baba yetu wa imani alishindwa kumtoa tajiri Katika mateso, haiwezekani kwa maombi yako wewe, kufanya jambo lolote kwa watu waliokufa tayari..

Ni wakati wa kuyachunguza maisha yako, usiishi kama mtu asiyejua majira na nyakati, tafakari mwenyewe, njia zako zinampendeza Mungu, jiulize wewe ni wa Mbinguni au kuzimu, ukiona upati jibu, ni wakati wako sasa, shetani ni mdanganyifu na maandiko yamemtaja kama baba wa huo uongo,

akiendelea kuziachia roho zake chafu za mapepo yafanye kazi ya kuwapotosha watu ili waamini kweli kuna maombi ya kumtoa mwovu matesoni, Kataa, anza kuishi maisha mazuri yenye utukufu kwa Mungu, mtumikie Mungu kwa nguvu zako zote, zidisha kuwahubiria wengine ili wamwamini Yesu wasiingie kuzimu,

Upotofu ni mwingi wanaoamini hivyo, hasa wa imani ya kikatoliki, kibiblia hakuna kupita toharani ndipo uingie Mbinguni, ukishaondoka duniani habari yako ndo imeishia hapo hapo, kama ni wambinguni utabakia huko huko, kama ni kuzimu nako utakuwa huko huko,

Waebrania 9:27

[27]Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

Mgeukie Kristo Leo,

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *