Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Katika nyakati hizi za Mwisho kumezuka kundi kubwa sana la viongozi ambao ni vipofu.. si kwamba hawaoni la! Kwa macho ya damu na nyama wanaona vizuri sana lakini katika roho ni vipofu hawaoni kabisa.
Na hii ni hatari sana maana wao ni vipofu na wanaowachunga vivyo hivyo nao ni vipofu. Na mwisho wa siku wote watatumbukia shimoni.
Kama mtu ulieokoka na unania ya kwenda Mbinguni kweli ni lazima uangalie sehemu sahihi ya wewe kula chakula chako cha Kiroho. vinginevyo ukikosea hapa basi jua kabisa upo katika hatari ya kutumbukia shimoni na huyo kiongozi wako.
Bwana Yesu analirudia hili jambo katika injili ya Mathayo mara tatu, na Luka jambo hili pia analinukuu vivyo hivyo na karibia injili zote ni jambo ambalo ni la kuwa nalo makini sana.
Bwana Yesu anasema..
Mathayo 15:14“Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
”
Unaona hapo anasema “Waacheni;hao ni viongozi vipofu wa vipofu….” Maana yake ni wengi viongozi vipofu na hao wanaowaogoza ni wengi..!
Na anasema “Waacheni..” maana yake watu ambao wameamua kuwa hivyo na wanafahamu kabisa wanachokifundisha hakipaswi kufundishwa..
Sasa tutakwenda kutazama sifa za viongozi vipofu ni zipi na kama ukiziona hizi ndugu mahali ulipo kimbia mara moja usiendelee kukaa hapo utaangamia.. salimisha roho yako.. kwa kutafuta mahali sahihi.
Sifa za viongozi vipofu..
1.Hakemei dhambi.
Kiongozi kipofu hakemei dhambi kabisa. Atakuhubiria Habari za kukufariji tu wala hatakwambia ukweli atakuhubiria maneno laini laini tu siku zote.
Yeremia 6:14“Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.
”
Watakambia yote Yesu alishalipa ishi jinsi utakavyo wewe umeshamuamini Kristo umepigwa mhuri wa Mungu huwezi kupoteza wokovu. Ndugu yangu usidanganyike kabisa juu ya hili.
2.Hakufundishi mafundisho ya siku za Mwisho.
Viongozi vipofu hawakufundishi mafundisho ya siku za mwisho hawakuhubiri Habari za kurudi kwa Yesu Kristo(uwe tayariwakati wote na kutembea katika haki na kweli). Hawakwambii kama Kuna kitu kinaitwa unyakuo,watakutumainisha wakati bado ishi tu unavyoona wewe mtu asikuhukumu Yesu alishamaliza kazi Kalvari pale. Nk
3.Wanahubiri mafanikio ya mwilini tu nk.
Watu hawa watakuhuburia sana sana mafanikio ya mwilini tu wala si ya rohoni. Watakusomea na kukufudisha sana na kukutumainisha katika mambo ya mwilini na bahati mbaya hutafanikiwa kabisa..
Watakuhubiria hayo siku zote na kama hujajaa Roho Mtakatifu utaendelea kufurahia mabapo hata ukiyapata hayo yote ni hasara kubwa kwako.
Marko 8:36“Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?”
4.Wokovu ni wa milele.
Watakutumainisha kuwa wokovu ni wa milele(ni kweli Wokovu ni wa milele ikiwa utaendelea kutembea na Kristo ni wa milele kabisa) wala huwezi ukaupoteza wakovu watakupa vifungu vyote lakini ni uongo maandiko yanaweka wazi sehemu nyingi (Waebrania 6, 2 Petro 2:20-22 nk)
Ndugu wokovu ni agano(ambalo ndani yake lina maagizo,utii nk) wokovu wa kweli pia utakufundisha kabisa kupitia Roho Mtakatifu kukataa ubaya..
Tito 2
11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Hivyo neema ya kweli ni lazima itakutofautisha 100% na watu au mambo ya kidunia..
Dunia yote itakuona kuwa ni mtu wa tofauti kabisa na itakutambua kuwa wewe ni nani..
Hivyo epuka mafundisho haya ni ya viongozi vipofu ambao kila unapotaka kupiga hatua wanakupa maneno ya kejeli kimbia kabisa sehemu hiyo.
Ziko sifa nyingine nyingine sana lakini hizi nimetamani tuzifahamu na kutafakari je mahali tulipo ni sahihi? Kama sivyo unasubiri nini? Usije ukasema hukuambiwa wala kuonywa.
Kumbuka huwezi kwenda nje na ufahamu sa kiongozi wako kama wewe hujaamua kutafuta maarifa mengine ya kutosha kumhusu Mungu na kweli yake ni ipi anayokutaka uijue?
Ukuwaji wa kiroho na kuogezeka zaidi katika kumjua Mungu unakutegemea wewe hapo.. kumbuka wokovu ni bure kabisa lakini unapookoka ni jukumu lako kumtafuta Mungu.
Hizi ni nyakati za Mwisho je unaishi kwa kuukomboa wakati? Je una shauku ya kwenda siku ile kwenye karamu ya mwana kondoo? Kama ndio kila siku ishi kwa kuukomboa wakati una usiwe ni mtu wa kupokea kila aina ya mafundisho zama hizi ni za uovu na utendaji kazi wa Shetani uko juu sana kuliko unavyodhani..
Usipoamua kutafuta maarifa ya kutosha kuhusu Mungu mwisho wa siku atakunasa tu..
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.