Je sadaka ya kinywaji ipoje?
Katika agano la kale ‘Divai’ peke yake ndiyo ilikuwa sadaka ya kimiminika iliyotolewa mbele ya Mungu..
Walawi 23:13 “Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na SADAKA YAKE YA KINYWAJI ITAKUWA NI DIVAI, robo ya hini”.
Sadaka hii ya kinywaji inatajwa pia katika vifungu vufuatavyo
Kutoka 29:40, Kutoka 30:9, na Walawi 23:18, Hesabu 6:15, Hesabu 15:6 na Hesabu 28:17
Swali la kujiuliza ni kwa nini ilikuwa DIVAI na sio kitu kingine?
Kwanza tutambue kuwa Divai haikupelekwa madhabahuni kwa ajili ya ulevi bali ilitumika kama nishati. Katika sheria ambazo Bwana alimwambia Musa awaagize wana wa Israeli ilikuwa ni pamoja na kutoa sadaka ya kinywaji ambayo ni Divai. Watu walipeleka Divai kwa kuhani, kisha kuhani aliingia nayo ndani ya hema na kuchukua sehemu ndogo ya Divai na kuimwaga juu ya madhabahu na kisha huweka unga mwembamba na tayari huwasha moto juu yake.
Sadaka hii ilianzia wapi?
Yakobo ndiye aliyeanza kutoa sadaka ya namna hii pale Betheli baada ya kutokewa na Mungu, kama tu sadaka ya Zaka ilivyoanzishwa na Ibrahimu alipokutana na Melkizedeki na baadae ikawa sheria kwa wana wote wa Israeli ndivyo ilivyokuwa hata katika sadaka ya kinywaji..
Mwanzo 35:9 “MUNGU AKAMTOKEA YAKOBO TENA, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.
10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.
11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.
13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, AKAMIMINA JUU YAKE SADAKA YA KINYWAJI, AKAMIMINA MAFUTA JUU YAKE.
15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.”
Je sadaka hii inawakilisha nini kwa sisi wa agano jipya?
Sadaka hii inawakilisha ‘damu ya Yesu’ ambayo alimwagika pale msalabani kwa ajili yetu mara moja tu. Damu ya Yesu inafananishwa na divai,
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, INAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU”.
Tunaona hapo kile kikombe kiliwakilisha damu ya Yesu iliyomwagika pale Kalvari tena ni ufunuo wa sadaka ya kinywaji ambayo ilimiminwa juu ya madhabahu, Na pia ilitoa ufunuo wa meza ya Bwana..
Bwana Yesu akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.