Je umetambua kuwa we ni shujaa wa Bwana?
Kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia, utakuwa unafahamu ile habari ya Gideoni alipoitwa na Bwana, biblia inatuonyesha kuwa Gideoni alikuwa ni shujaa lakini hakujitambua mpaka alipotokewa na malaika wa Mungu na kujulishwa kuwa we ni shujaa. Hebu turejee biblia…
Waamuzi 6:11-16 Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
[12]Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA YU PAMOJA NAWE, EE SHUJAA.
[13]Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
[14]BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?
[15]Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.
[16]BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.
Yamkini, wewe ni Gideoni wa leo, na Bwana anasema na wewe upate kusikia wito wake na kufahamu kuwa wewe ni shujaa na Bwana anataka kukutumia pasipo kujalisha udogo wako, au hali yako ya kiroho au kimwili…kwamba unaelimu au hauna, una kipato au hauna. Kumbuka Gideoni alikuwa anapepeta ngano, alitoka kwenye ukoo wa kimaskini, na pia alikuwa mdogo kati ya ndugu zake, lakini ndiye ambaye Bwana amemuona ni shujaa akamchagua.
14]”BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. JE! SI MIMI NINAYEKUTUMA?
[15]Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.
[16]BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.”
Bwana anapokuita, hangalii cheo chako, wala Elimu yako, wala jamii yako au ukoo wako, wala hangalii unajua sana au unajua kidogo, wala haangalii umri wako kwamba ni mdogo au mkubwa, na hali kadhalika haangalii unayo fedha au hauna. Zaidi Bwana huwa anapenda kuvichagua vile vitu vinyonge na dhaifu ili ajiinulie utukufu.
1 Wakorintho 1:26-28 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
[27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
[28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
Hivyo katika udogo wako, udhaifu wako, unyonge wako tambua kuwa we ni shujaa na Bwana anakuita umtumikie katika hali hiyo hiyo uliyonayo ili atukuzwe kupitia wewe. Huna haja ya kusubiri mpaka uende kusoma vyuo vya biblia ndio uwe mnjilisti, au uwe na fedha ndio umtumikie Bwana.. fahamu kuwa Bwana anakuona we ni shujaa sasa katika hali uliyonayo, alimwambia Yeremia..
“..Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.” (Yeremia 1:7)
Umekuwa ukijiona hujafikia bado viwango vya kutumika mbele za Mungu, mpaka utakapopitia pengine madarasa Fulani au chuo fulani au hatua Fulani kama za mchungaji wako au mwalimu wako, hiyo ni kweli kabisa, lakini leo Bwana amekuchagua wewe sasa katika udogo huo, ukamtukuze katikati ya mataifa. Hivyo Ndivyo ilivyompendeza yeye.. alisema hivi.
“Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, UKAWAFUNULIA WATOTO WACHANGA. 26 Naam, Baba, KWA KUWA NDIVYO ILIVYOPENDEZA MBELE ZAKO.(Mathayo 11:)
Unaona? Hivyo ndugu ikiwa utausikia ujumbe huu, ikiwa utasikia wito wa Mungu ndani yako, usikawie kawie, wala kujiuliza uliza mara mbili eti mimi nafaa, au nitaweza?, ingia gharama ya kumfuata Kristo, jitwike msalaba wako, umfuate sasa, neema hiyo haitadumu milele juu yako ukichelewa chelewa shetani naye yupo pembeni kutaka kukutwika mizigo yake, au akupande ili akutumie katika mambo yake maovu, wakati ndio huu uusikiapo ujumbe huu.. chukua uamuzi sasa. Kwasababu yeye mwenyewe alisema..
Mathayo 28:29 “JITIENI NIRA YANGU, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
Sasa usisubiri shetani akutie nira yake ngumu katika uchanga wako, huu ni wakati wa kusema mimi na YESU tumefunga pingu za maisha milele..Na kuanzia sasa namaanisha kumfuata YESU katika hali zote zitakazokuja mbele yangu. Na hakika atakuangazia wema wake kwa wakati wake aliouweka juu yako.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.