Je! Utoaji wako unamgusa Mungu?.

Biblia kwa kina No Comments

Je! Utoaji wako unamgusa Mungu?.

SEHEMU YA TANO(05)... Sehemu ya mwisho.

Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe karibu katika sehemu ya mwisho wa somo letu hili.

Katika kanuni namba nne tulijifunza juu ya kanuni ya kujidhabihu.  Na leo katika sehemu ya mwisho tutajifunza kanuni muhimu sana.

#5 kanuni ya kubarikiwa.

Siku zote “Matokeo ya utoaji unaomgusa Mungu ni baraka.”

Katika maisha ya kawaida kila kitu kinachofanyika kina matokeo yake. Yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Vivyo hivyo na katika utoaji unaomgusa Mungu.

Utoaji unaomgusa Mungu ni ule unaozingatia kanuni nne za mwanzo tulizojifunza.. kanuni ya umiliki, kanuni ya upendo, kuchagua, kujidhabihu.

Baraka ni upendeleo wa Ki-Mungu anaoupata mtu baada ya kutii na kufanya maagizo aliyoagizwa na Mungu. Maandiko yanasema katika….

Kumbukumbu la Torati 28

1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;

2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.

Hivyo baraka si muujiza, si bahati au matokeo ya maombi mengi sana. Ni matokeo ya kusikia kwa bidii na kutenda yale uliyoagizwa kufanya. 

Siku zote tambua hili “Kutoa ni kuwekeza si kupoteza. ”

Kama unatoa kwa uaminifu bila kujali vipindi na nyakati basi tambua kabisa unawekeza ambao uwekezaji huo ni wa kudumu yaani wa milele utakusaidia hapa duniani na kule mbinguni.

Hata leo unapopanda mazao unawekeza katika aridhi. Na unatarajia kuvuna zaidi ya kile ulichokipanda kwa sababu kile ulichokiwekeza kinazaa zaidi ya kile ulichokipanda.. naomba paelewe hapa na patafakari.. unapanda mbegu moja ya muhindi au mbili lakini mbegu zaidi ya 100 zinazaliwa hapo.. Haleluya.

Maandiko yanasema…

Mithali 11:24 “Kuna atoae kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini.”

Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mtakachopimiwa.”

 

Katika sura hii tutajifunza baraka kuu tatu ambazo tunazipata kutoka kwa Ibrahimu. 

#1 Baraka ya kukutana na Mungu. 

Hii ni baraka ya kwanza kabisa kama utatoa utoaji unaomgusa Mungu basi ni lazima utakutana na Mungu tu. Maana katika utoaji wa kweli Mungu yupo mahali hapo. Na hapo ndipo zilipo baraka.

Ukisoma Ibrahimu alikutana na Mungu katika utoaji wake hebu tusome…

Mwanzo 22:11“Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.”

Mungu anamtokea Ibrahimu baada ya siku tatu kavu bila kuona uwepo wake(kuna wakati Mungu atakaa kimya unapotoa lakini haimaniishi hakuoni ama hayupo ndugu yupo na baraka zako zipo usichoke).

Mungu anaweza kukutana na watoaji kwa namna mbali mbali.

2.kwa kuwapa mahitaji yao.

2 Wafalme 4:8-17 .Mwanamke aliyekuwa hana mtoto, alijitolea yeye pamoja na familia yake kumhudumia Elisha mtumishi wa Mungu. Baadaye tunaona Mungu anakutana na hitaji lake la mtoto kupitia kwa Elisha.  Si hawa tu ipo mifano mingi.

Kornelio, baada ya sadaka zake kufika kwa Mungu, Mungu alimtokea na kumwongoza kuupata wokovu. Mara zote Mungu hukutana na mahitaji ya watoaji. Inawezekana una mahitaji mengi umeomba sana na bado hujajibiwa. Unaweza kuamua kumtolea Mungu sadaka nzuri naye atatokea kwako nakukupa haja ya moyo wako.

3.kwa kujibiwa maombi yao.

Ibrahimu alikosa mtoto kwa kipindi cha miaka mingi na alikuwa akiomba na siku moja wageni watatu wanakuja kwake na kuwakaribisha na mwisho kabisa Ibrahimu anajibiwa maombo yake kwa kuambiwa mwakani majira kama haya Sarah atapata mtoto.

Njia mojawapo ya kujibiwa maombi ni kutoa.” Huenda wewe ni muombaji mzuri ,unafunga nk lakini ni mzito katika kutoa fanya hivyo utaona milango inavyofunguka. Simaanishi kutoa unamshawishi Mungu la.

4.kwa kutatua matatizo yao.

Mungu anatatua matatizo ya watu wanaomtolea pia..

Vitabu vya injili vinaeleza habari za mwanamke mmoja aliyekuwa anateswa na dhambi kwa muda mrefu. Mwanamke huyu aliamua kuchukua mafuta ya thamani kubwa (Marhamu) na kuanza kumpaka Yesu kwa nywele zake.

Huu ulikuwa ni utoaji mkubwa katika historia ya Biblia. Na matokeo yake tunaona mwanamke huyu anasamehewa dhambi zake na kuwa huru mbali na tatizo hilo (Luka 7:36-50)

Utoaji unaweza kuwa sababu ya wewe kuwa mbali na tatizo lako. Chukua hatua.

Pia Soma Habari ya Dorcas (Tabitha) kupitia utoaji wake anapata nafasi ya kuishi Mara ya pili baada ya kufa.

2.kustawi.

Baraka nyingine ambayo ni matokeo ya utoaji ni kustawi. Kustawi ni hali ya kuwa na kila kitu unachokihitaji.

Au ni hali ya kutokuwa na upungufu.  “Kila unapotoa ujue kuwa unafungua mlango wa kupokea kitu kipya.” 

Ni ngumu kumkuta mtoaji akiwa ana upungufu, kwa sababu kila anapotoa hupokea zaidi ya kile alichotoa na hivyo wakati wote hujikuta akiwa na vitu vingi.

anapokuwa na vingi huendelea kutoa zaidi na kupokea zaidi. Na hayo huwa ndiyo maisha ya watoaji; Kumbuka kile biblia inasema katika;

Mithali 11:24-25 “Kuna atoae kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini. Nafsi ya mtu mkarimu”

3.Kuwa baraka kwa wengine.

Mungu amekusudia kila mtu awe baraka kaa watu wengine kwa njia ya utoaji”

Zaidi ya kukutana na Mungu pamoja na kustawi, Mungu amekusudia watoaji wawe baraka kwa watu wengine. Na jambo hili si kwa mwanadamu tu bali kwa kila kitu kilichopewa uwezo wa kutoa.

Kila kitu kilikusudiwa kiwe baraka kwa vitu vingine. Kwa mfano, Ng’ombe hutoa maziwa lakini hakuna siku utamkuta anakunywa maziwa yake isipokuwa watoto wake

au wanadamu. Miti yote ya matunda huzaa matunda kwa wakati wake lakini hakuna mti hata mmoja ambao huyatumia matunda yake kama chakula.

Mungu mwenyewe alimtoa Yesu Kristo kwa ajiri ya ulimwengu wote na tunaona Kristo amefanyika baraka ulimwenguni kote kwa kututoa katika hukumu ile itishayo zaidi sana katupa uzima wa milele na kututoa katika utumwa wa shetani na katuheshimisha kuliko malaika na kuliko kitu chochote duniani.

Huyo ni Yesu Kristo tunaemuabudu.. Haleluya.

1Yohana 4:10 “Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.”

Hana. Wasomaji wa biblia tunaona anamtoa Samweli kwa Bwana na anafanyika baraka katika taifa zima la Israeli wakati ambapo hapakuwa na mafunuo dhahiri ila kwa sababu ya uaminifu wa Hana kumtoa mwanae tunaona Israeli inaongozwa na Samweli kwa kipindi kirefu huku akiacha Alama kubwa sana katika taifa.

 

Ipo mifano mingi ya kina Daudi,Dorcas nk isingetosha kuielezea hapa yote.. hivyo amini kabisa unaweza kuwa baraka kwa wengine na watu wakafurahi na kumtukuza Mungu kwa ajiri yako..

Hebu tafakari mtu anamshukuru Mungu kwa ajiri yako unafikiri Mungu atakaa kimya?

Unawezaje kuwa baraka kwa wengine?.

Nirahisi na inawezekana Kitakachokufanya uwe baraka kwa wengine ni uwezo wako wa kutoa kila ulichonacho kwa lengo la kuboresha maisha ya watu wengine. Usiwe mbinafsi, tumia kila fursa unayoipata kutoa na kujitoa kwa ajili ya wengine.

Kumbuka, ulipewa hivyo ulivyonavyo ili viwe sababu ya wengine kubarikiwa.”

Kama una kipaji kitumie kuwaendeleza wengine. Kama una fedha itumie kumsaidia mtu mwenye uhitaji. Kwa kila ulicho nacho ambacho unahisi kinaweza kumsogeza mwingine mbele kitoe kwa kusudi hilo. Kwa kufanya hivyo tu wewe utakuwa miongoni mwa watu ambao ni Baraka kwa wengine.

Nimekuombea uwe Baraka kwa wengine katika Jina la Yesu Kristo.

Nikupongeze na kukuombea baraka nyingi kwa Mungu kwa wewe ambaye umefatilia somo hili tangu mwananzo na hata sasa Mungu akubariki sana.

Ubarikiwe sana.

 

Mawasiliano: 0613079530.

@Nuru ya Upendo.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *