
KAMA MAMA YA MTU ALIVYO, NDIVYO ALIVYO BINTI YAKE.
“Like mother, like daughter.”
Unaelewa maana ya hii sentensi?
Biblia inasema katika..
Ezekieli 16:44 “Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, KAMA MAMA YA MTU ALIVYO, NDIVYO ALIVYO BINTI YAKE”.
Hii ikiwa na maana kuwa tabia za mama ni sawa na tabia za mtoto na kinyume chake pia.
Sasa ukirudi nyuma kwenye hili andiko, utaona Mungu alikuwa anazungumza na taifa lake la Israeli kama mwanamke aliyemuacha mume wake na kwenda kufanya ukahaba huko nje na wanaume wengine.
Israeli walimuacha Mungu wa kweli na kugeukia kuabudu miungu ya kipagani, wakasahau wema na fadhili BWANA alizowatendea.
Lakini biblia inasema kama mama wa mtu alivyo ndivyo alivyo binti yake.
Tunasoma kitabu cha Ufunuo sura ya 17 biblia inasema..
Ufunuo 17:1 “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.”
Kama tunavyojua mwanamke katika biblia anawakilisha KANISA, Sisi wakristo tunatambulika kama BIBI-ARUSI wa KRISTO, (2Wakoritho 11:2 Paulo anasema
“..Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo BIKIRA SAFI. “) Na pia..
Ufunuo 19:7 inasema..” Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na MKEWE amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
Pia Taifa la Israeli Bwana alilitambua kama MKE WAKE” [soma ezekieli16:1-63, ezekieli 23] utaona jambo hilo. Hivyo mahali popote Mungu anapozungumza juu ya kundi la watu wake huwa analifananisha na mwanamke.
Lakini hapa tunaona mwanamke mwingine ametokea ambaye anaonekana ni KAHABA, amelewa kwa DAMU za watakatifu na za mashahidi wa YESU, na tena wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake ana jina limeandikwa, la SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
Hivyo tunaona tabia ya huyu mwanamke (ambaye anawakilisha KANISA fulani) kuwa ni KAHABA, Na kama tunavyofahamu kanisa la KRISTO haliwezi kuwa kahaba, kwasababu ni BIKIRA SAFI, na haliwezi kuua watakatifu wa Mungu, kwasababu lenyewe ni TAKATIFU, Hivyo hili Kanisa haliwezi kuwa lingine zaidi ya KANISA KATOLIKI chini ya uongozi wa PAPA.

Huyu ndiye mama wa makahaba!! (Kwa urefu zaidi kuhusu siri ya hili kanisa tuandikie ujumbe inbox).
Na kwanini tena ni MAMA WA MAKAHABA?, Ikimaanisha anao mabinti ambao nao ni makahaba, na yeye mwenyewe anafanya ukahaba..Na kama yeye ni kanisa ni wazi kuwa watoto wake nao watakuwa ni makanisa/madhehebu na wote wanafanya ukahaba. Hiyo ndio maana ya maneno haya..
“kama mama wa mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake”.
Kanisa linalofanya ukahaba kibiblia ni kanisa linaloabudu sanamu, na kuacha sheria za Mungu.
Hivyo kama upo miongoni mwa watoto wa kahaba yaani mwana -mwadhehebu na ulikuwa hauna maarifa haya, basi leo umejua, hivyo usiendelee kukaa hapo, toka katika mafundisho hayo ya kuabudu sanamu, kusali rozali, kuombea wafu, na mafundisho mengine mengi yanayopingana na Neno la Mungu.
Fuata Neno la Mungu usifuate mapokeo ya watu.
Makanisa yanayohubiri injili ya mafanikio tu. Na kukwambia kuwa uthibitisho wa Mungu kuwa yupo na wewe, ni kuwa tajiri …JIHADHARI NA HILO KANISA! Ni kanisa kahaba.
Makanisa yanayohubiri ujumbe wa kutoa tu, na kuacha mafundisho ya adili kama upendo, utakatifu na imani,,,,JIHADHARI NA HILO KANISA KWA USALAMA WA MAISHA YAKO YA MILELE.
Kanisa lisiloruhusu karama za Roho kufanya kazi, kama uponyaji wa kiungu, unabii, lugha, miujiza n.k. jua hilo sio kanisa la Kristo bali ni kanisa (mtoto) wa yule kahaba mkuu. CHUKUA TAHADHARI!.
Kanisa lisilokufundisha wala kugusia kujiandaa kwenda katika unyakuo…KUWA MAKINI!
Toka katika madhehebu yanayokuambia Mwanamke anaruhusiwa kuvaa suruali, nguo fupi, na kujipamba kwa mapambo ya kiulimwengu hilo ni kanisa la shetani, hawakwambii ukweli kwasababu anayeabudiwa humo ni shetani! Na shetani analohitaji ni kuipeleka nafsi yako kuzimu! Hilo tu!!
Ujumbe wa saa hii ni kutoka katika mapokeo ya ki-Madhehebu? Na kurudi katika Neno la Mungu.
Ufunuo wa Yohana 18:4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
[5]Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.
Maran atha(Bwana Yesu anarudi)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.