Kuna utofauti gani kati ya damu ya Yesu na jina la Yesu?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze Maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

Pengine ulishawahi kujiuliza hili jambo na usipate majibu kamili, au lilishawahi kukuletea sintofahamu ndani yako, ni kuhusiana na damu ya Yesu na jina la Yesu,zidi kusoma nakala hii ikupe uelewa zaidi wa kimaandiko..

Ni sawa tuchukulie uhalisia wa maisha ya kawaida tu, hakuna mtu asiyekuwa na jina, kila mmoja analo,ila jina linaelezea yeye ni nani, au ana nafasi ipi, nguvu yake ni ipi, heshima aliyonayo,au cheo chake ni kipi, sasa haya yote hauyatambui kwa kumwangalia uso bali kwa kuangalia jina lake, tuchukulie mfano raisi wa nchi,tunamtambua na nafasi zote hizi kwa sababu ya jina lake, kwakuwa yeye ndiye mwenye jina lililokuwa kubwa kupita watu wote..na wenye vyeo vikubwa hutambulika kwa majina yao..

Lakini Damu ya mtu haielezei vyeo,au nafasi ya mtu bali inaelezea asili ya huyo mtu ni nini, inamuelezea yeye na chanzo cha familia aliyonayo,uzima wake alionao, na jinsi gani anavyoweza kurithisha baadhi ya vitu kupitia damu yake, na urithi wake kwa ujumla..

Na kila Mwanadamu lazima anayo damu lakini pia analo jina..

Mambo haya pia yapo kwa Bwana Wetu Yesu Kristo, yeye aliyezaidi ya raisi yoyote duniani kote, Bwana Yesu ana jina lakini pia anayo damu kama na sisi tulivyo, kwasababu damu inafichua undugu wa mtu, sasa wale wote walimpokea Yesu Kristo,waliozaliwa mara ya pili, hao tayari ni Ndugu wa Bwana, damu Moja..

Luka 8:21

[21]Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.

Umeona hapo,

Ukishakuwa ndugu wa Yesu Kristo maana yake unakuwa na mamlaka ya kuwa karibu na yeye au hata kuomba chochote kwa jina lake ukapokea, ni sawa na mtu wa kawaida tu akataka jambo fulani Kutoka kwa kiongozi wa nchi, inaweza ikamchukua muda mrefu kusikilizwa au kupokea majibu yake pengine hata asikipate kabisa, lakini hiyo ni tofauti na mtoto wa kiongozi huyo, yeye chochote atakachokitaka anao uwezo wa kukipata kwa muda wowote kwasababu kuna damu,au undugu kwa kuwa anayetawala ni baba yake, sasa kilichomuwezesha huyu Mtoto wa kiongozi ni Damu ilitoka kwa jina la babaye ikampelekea yeye kusikilizwa sana..

Maandiko yanasema Damu ya YESU KRISTO inanena mema kuliko ile ya habili, hii ikituonyesha kitendo cha wewe tu kufanyika mwana wake,yani kuwa Damu yake, tayari unakuwa ni uthibitisho unahitaji kutendewa mema yote hata pasipo kuomba sana, linakuwa ni jukumu la Baba wa Mbinguni kukupa chakula, kukupigania dhidi ya mabaya,kukulinda na kukuhakikishia ulinzi nyakati zote, na hata ukiwa Katika kuomba kwako utapokea majibu ya haraka kwasababu utalitumia jina lake kupokea baraka zote.. ukiwa nje ya Yesu ni ngumu kupokea kwasababu bado hujawa damu moja,sio mwana wake,ni bahati nasibu kupokea..

Yohana 14:13-14

[13]Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

[14]Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

UMEFANYIKA DAMU MOJA na BWANA, Umeokoka,

Muda ndio huu hautajirudia tena ndugu, jiulize wewe ni damu moja na Mungu, umefanyika kuwa mwana wake, kama bado hujaokoka ni vigumu kuwa karibu na Mungu,ni vigumu kupokea baraka za ki-Mungu,ni vigumu kupata upendeleo kwake,yeye huwaangalia wali wake na kuwashushia mema yote, na baraka kubwa aliyowapa waliofanyika Watoto wake ni muwarithisha Uzima wa milele, jambo ambalo ni gumu kulitoa kwa ambaye sio mwanao,

Warumi 8:28-29

[28]Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

[29]Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

Msingi mkubwa ni wewe sasa kufanyika kuwa mwana wa Mungu, Kumbuka wana wa Mungu wanaurithi Ufalme walioekewa tayari na Baba yao wa Mbinguni lakini wale waliokataa watatupwa kwenye ziwa la moto pamoja na baba yao shetani aliyeasi tokea hapo kwanza,

Nafasi unayo ya kutengeneza, ni kwa kutubu dhambi zako zote ukimaanisha kabisa kuziacha,unaacha kunywa pombe,unaacha uzinzi, Ushirikina, kwenda kwa waganga,unaacha wizi, ulikuwa unavaa nguo za utupu unazitupa, hereni, mawigi yote,kucha bandia,vyote vinavyomchukiza Mungu,

Ukiyatenda hayo,jambo lililobaki ni wewe sasa kubatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, utapokea Roho Mtakatifu atakayekuongoza na kukufundisha ndani yako njia za Bwana

Yohana 3:5

[5]Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Bwana akusaidie kuchukua maamuzi sahihi,

Shalom..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *