SWALI.. Kwa nini Mungu aliikataa sadaka ya mazao kutoka kwa kaini na akaikubali sadaka ya wanyama kutoka kwa Habili?
Je wanyama ni bora kuliko mazao mbele za Mungu?
JIBU..Tusome
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”.
Mungu aliikataa sadaka ya Kaini si kwa sababu hapendi mazao, hapana. Pengine sadaka ya mazao inaweza kuwa nzuri ukilinganisha na wanyama ambao wanahusika na kumwaga damu. Sababu ya Mungu kuikataa sadaka ya Kaini tunaiona katika mstari wa 3 na wa 4..
“Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta WAZAO WA KWANZA wa wanyama wake na SEHEMU ZILIZONONA za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;”
Habili alipeleka wazao wa kwanza wa wanyama walionona, lakini nduguye Kaini hakupeleka sehemu ya kwanza ya mazao yake bali alipeleka sadaka dhaifu kama yalikuwa mahindi yawezekana alipeleka yale yaliyoharibika au kama yalikuwa matikiti basi yalikuwa yamekaribia kuoza na yale mazao mazuri aliona yanamfaa yeye kuliko Mungu aliyempa vitu vyote bure.
Yeye alimuweka Mungu katika nafasi ya pili na mali zake zikawa nafasi ya kwanza, Mungu pia alimfanyia hivyo hivyo akamuweka nafasi ya pili na nduguye akamuweka nafasi ya kwanza.
Labda Kaini hakuwa na uelewa juu ya utoaji na kwa jinsi Mungu wetu alivyo na upendo aliamuonya na kumfundisha namna ya kutoa sadaka nzuri ili na yeye akubaliwe kama ndugu yake lakini Kaini hakumsikiliza Mungu badala yake akaenda kumuua ndugu yake jambo ambalo lilikuwa baya zaidi mbele za Mungu.
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? “
Tunajifunza nini katika hilo?
Tunachojifunza hapo ni kuwa Mungu anaangalia kile tunachomtolea tena anatoa hukumu kulingana na kile tulichotoa, neno linasema ‘Hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake utakapokuwepo (Mathayo 6:21). Ikiwa hazina yako ya kwanza hujaiweka kwa Mungu basi moyo wako pia haupo kwa Mungu kama tu alivyokuwa Kaini. Hazina ya Kaini haikuwa kwa Mungu ndio maana hata moyo wake haukuelekea kwa Mungu.
Kama unataka kujua moyo wako upo kwa Mungu basi angalia namna unavyotoa kwa kufanya hivyo utajua wewe ni mtu wa namna gani. Hivyo basi kama hutoi sadaka unafanya dhambi, uwe tayari kumtolea Bwana bila kuambiwa. Mtolee zaka na sadaka zilizonona ili moyo wako uwe kwake na upate baraka zake.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.