SWALI...Kwa nini tunatoa sadaka? Kuna muhimu gani wa kutoa sadaka? Je ni dhambi usipotoa sadaka?
JIBU..Kutoa ni wajibu wa kila mtu aliyemwamini Kristo iwe ni kutoa sadaka au kitu kingine chochote. Mtu asiyetoa bado hajabadilishwa moyo wake na maisha yake yapo mbali na Mungu.
Sisi tunatoa sadaka kwa sababu hata tulivyonavyo tumepewa na Mungu, yeye ndiye alianzisha utoaji, ametupa vitu vingi ambavyo hatuvilipii kitu chochote. Na sisi tumeumbwa kwa mfano wake, Mwanzo 1:26.
Ikiwa mtu hatoi basi hana ule uungu ndani yake kwa sababu kutoa ni sifa kubwa ya Mungu. Ametoa vitu vingi kwetu, uzima na maisha ametupa bure tena akamtoa mwanae wa pekee ili tupate uzima wa milele, Yohana 3:16.
Hivyo sisi pia inatupasa tuuige mfano wake, tufanane naye.
Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Kutoa ni ‘wajibu’, haina haja ya kulazimishwa au kukumbushwa juu ya jambo hili, yakupasa ujue ni wajibu wako kutoa. Unapotimiza wajibu wako basi utapata faida.
Moyo wako ukiwa mgumu au mzito kumtolea Mungu na pengine unawaza kwamba utapoteza unavyotoa basi omba msaada kwa Mungu aiondoe hiyo roho ndani yako ili usiwe kama Kaini ambaye aliona hasara kumtolea Mungu akaona kama amelazimishwa kisha akatoa sadaka dhaifu ambayo ilikataliwa mbele za Mungu.
Kila ulichonacho Mungu amekupa bure kwa nini moyo wako uwe mzito kumtolea sehemu ya kumi tu na zile 9 uchukue? Kama huwezi kutoa kidogo kama hicho basi kutakuwa na shida ndani yako.
Ardhi unayokanyaga, pumzi unayovuta vyote umepewa bure hata mwanga wa jua unaotumia umepewa bure
Wakati unatumia pesa kuwalipa tanesco pesa kwa ajili ya kupata mwanga mdogo tu na bado unaumia kumtolea Mungu tena bado umamuibia, ukiwa na moyo wa namna hiyo huwezi kumlingana Mungu hata kama wewe ni muombaji mzuri bado utaonekana kuwa mnafiki mbele za Mungu.
Usiache kumtolea Mungu tambua kuwa huo ni wajibu wako, yapo madhara kama hutafanya hivyo, Mathayo 25:41-46.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.