kwanini mwokozi hakuendelea kuitwa imanueli badala yake akaitwa Yesu?

Maswali ya Biblia No Comments

Ni siku nyingine Bwana ametupa tuyatafakari Maneno yake, karibu..

JIBU

Ukisoma maandiko kwenye kitabu cha Isaya,utagundua unabii alioutoa nabii isaya kuhusu jina la mkombozi atakayekuja ulimwengu lilikuwa ni Imanueli (Isaya 7:14) kuonyesha kwamba ni lazima litimie hilo, kwasababu maandiko hayawezi kusema uongo..

Lakini tuendelee kusoma zaidi ili tuzidi kujifunza kama wanafunzi wanaotamani kupata uelewa..

Tusome hapa,

Mathayo 1:19 “Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,

23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; NAO WATAMWITA JINA LAKE IMANUELI; YAANI, MUNGU PAMOJA NASI”.

Umeona hapo mstari wa 23, mwishoni, amelitaja lile jina husika tuliloliona kwenye unabii wa Isaya lakini hakuishia hapo tu, ameendelea mbele zaidi kukupa tafsiri ya hilo neno ni nini, yani MUNGU PAMOJA NASI, na uhalisia upo kwenye hii tafsiri ya hilo neno na sio kwenye hilo jina, kwasababu sisi ndio tutakaomwita Mungu pamoja nasi, sawa sawa na ujumbe wa malaika alioutoa kwenye huo mstari wa 23, na bado pia hilo sio jina lake halisi, jina lake litakuwa ni Yesu, yaani YEHOVA MWOKOZI,

Limekuja kujihidhirisha hili kwasababu tumeshafahamu Yesu Kristo ni nani kwetu na kwa ulimwengu, sio Mwokozi tu bali ni Mungu mwenyewe aliyeaumua kuchukua mwili akaja duniani kwa ajili ya kuleta ukombozi, akaishi na Mwanadamu,akatembea nae,na kuzungumza..

Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu”…..

14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.

1Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”

“Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili”(Wakolosai 2:9) .

“tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;(Tito 2:13)

Ukiyafahamu haya kwanini usiwe na ujasiri wa kumwita Bwana Yesu,mana ndiye Mungu wetu, Mwokozi Wetu,kimbilio letu na msaada tele, yaani Imanueli, mgeukie leo Bwana Yesu,akusamehe dhambi zako akutakase upokee Roho Mtakatifu, saa ya Wokovu ni sasa..

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *