Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu wetu ambalo ndilo taa yetu..
Hakuna jambo kubwa na la muhimu kama hatma yako ya mwisho ni nini, wengi tumekuwa tukichezea maisha yetu, kwa kufanya tunayoyataka, ila kiuhalisia sivyo Mungu anavyotaka tuwe, kumbuka maisha unayoyaishi leo ndio jawabu la kesho yako jinsi litakavyokuwa, huna budi kujitafakari sana kila wakati ili utengeneze maisha yako Katika mapenzi yaliyo mema,..
Hili ni swali ambalo unalopaswa kujiuliza sana, kwasababu watu wengi wamekuwa na mashaka pale wanapoulizwa wana uhakika gani kama wataenda Mbinguni, au wakifa wataenda mbinguni, majibu yao yanakuwa na kusita sita yasiyokuwa na majibu kamili, mwingine atakumbia, Mungu ndiye anajua nitaenda wapi, au mimi sio Mungu siwezi kujihesabia haki, na wengine wanasema kabisa hawajui wataenda wapi, jambo ambalo ni hatma mbaya sana ya maisha yako, tofauti na wale wenye uhakika ni wachache wanaoweza kujibu..
Lakini kigezo cha wewe kuwa na uhakika wa kwamba utaenda Mbinguni unatokana na nini, na hapa pia kila mmoja atakuwa na majibu yake, mwingine atasema kwasababu nasaidia sana yatima, mwingine naishi kwa kutenda matendo mazuri, lakini uhalisia sivyo..Ukipata elimu ya Neno la Mungu itasema kila aliye mwana wa Mungu lazima awe na hakikisho ndani yake kama hata akiondoka duniani leo lazima aende Mbinguni na kwamba anao uzima wa milele ndani yake..
1Yohana 5:13 “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu”.
Sasa uhakika huu hauji kwa kusema kwa vinywa vyetu wenyewe, kwasababu anaouleta huu uhakika ni Yesu mwenyewe endapo utakuwa umekamilishwa na yeye mwenyewe, wengi hawafahamu kuokoka ni neno pana, sio kusema tu nimeokoka nampenda Yesu, lazima uende zaidi ya hapo, na kuokoka sio sala ya toba, unaweza ukaisema mwaka mzima na usione badiliko lolote ndani yako,
kwa sababu kazi anayoifanya Bwana ni kufanya kuleta badiliko la ndani kabisa ambalo sasa hilo halitahitaji ufosi kujibu bali mwenyewe anakuongoza na kukuhakikishia kuwa unao uzima wa milele bila kusumbuka au kujiuliza uliza..
Na hakikisho hilo linakuja ndani ya mtu kwa kuyatii maagizo yote ya Bwana,sio kutubu tu, maandiko yanasema aaminiye na kubatizwa ataokoka, hapo lazima ukabatiwze ubatizo ulio sahihi,ukilijua hilo unawahi na kuutafuta ubatizo haraka sana,
yapo maagizo mengi,
Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Jiepushe na Mambo yote maovu ambayo ni machukizo kwa Mungu, jiepushe na uzinzi, pombe,ulafi, acha kuvaa suruali kwa mwanamke, hereni, mawigi,tupa make up zote,na mambo yanayofanana na hayo, na unaanza kujikana nafsi na kuuchukua msalaba wako na kisha unamfuata Kristo,
Ukifanya hayo,utajikuta Kristo anaanza kukupa uhakika tu ndani, utajiona mwepesi na amani itaanza kuingia ndani yako, hata ukianza kujiuliza ukifa utaenda wapi,utaona hata usipojibu kwenye kinywa ila ndani kuna toa jibu lenye uhakika kwa kuwa Kristo ndiye anayekushuhidia..
Lakini tukienda kinyume na hayo maagizo,basi tufahamu huo uhakika hautaweza kuingia ndani yetu, hata tukijlazimisha tutajidanganya wenyewe, kwasababu kwenye kwenye Ufalme wa Mungu ni zaidi ya kusalishwa sala ya toba,ni zaidi ya kusema nimeokoka nampenda Yesu,ila kusikiliza na kukitendea kazi unachoambiwa kwenye neno lake na kutii..
Yohana 5:24 ‘Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani’.
Anza kuyatengeneza maisha yako sasa hivi kwasababu Neema ya Yesu Kristo bado ipo, kama ujaokoka ni wakati wako sasa, muda tulio nao ni mchache sana, Kristo anarudi kuwachukua walio wake, jiulize utakuwa wapi wewe? Maisha yako unayoishi yanaeleza ni wa Mbinguni au motoni,
Ndugu mrudie Bwana,ishi maisha matakatifu, mtafute Bwana anapatikana, yeye anawarehemu watu wengi kila wakati, aliniokoka mimi fahamu anataka akuokoe na wewe pia,
Bwana akubariki..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.